Thursday, April 12, 2012

“HEINEKEN CHAMPIONS PLANET” YAAHIDI RAHA NA MSISIMKO KWA WATEJA WAKE TANZANIA




“HEINEKEN CHAMPIONS PLANET” YAAHIDI RAHA NA MSISIMKO KWA WATEJA WAKE TANZANIA

•       “Heineken Champions Planet” inelenga kuwapa mashabiki wa Ligi ya Mabingwa ya  UEFA  burudani ya kipekee  kwa wateja wa Heineken


•       Heineken  imekuwa ikishirikiana na UEFA tangu msimu wa 2004/05 na itaendelea kuwa mfadhili mkuu wa mashindano haya hadi  mwaka wa 2014/15.

Dar es Salaam, April 11, 2012:  Bia ya kimataifa ya Heineken leo (jana) imetangaza uzinduzi wa "Heineken Champions Planet" itakayo wapa wateja wake nafasi ya kuangalia mashindano kabambe ua Ligi ya UEFA msimo wa 2011/2012.

Uzinduzi wa “Heineken Champions Planet”  unatokana na  mafanikio makubwa ya matembezi ya kombe la Ligi  ya UEFA  uliyo dhaminiwa na Heineken hapa nchini Tanzania na Kenya kutoka Machi 23  hadi  Machi 31. Katika kipindi hiki, kombe la UEFA lilikuwa nchini Tanzania kwa siku tatu kamili, watumiaji wa Heineken pamoja na wadau wa soka waliungana pamoja kushabikia  kombe hili la kifahari.

Ligi ya mabingwa ilianzishwa na UEFA mwaka wa 1992, na  inadaiwa na wengi kama  mashindano bora katika ulimwengu wa soka. Heineken imekuwa ikihusika na mashindano hayo kama mfadhili rasmi tangu msimu wa 2005/2006. Leo hii inaendelea kuwa mfadhili mkuu wa mashindano haya hadi msimu wa 2014/2015.


“Heineken Champions Planet” inayozinduliwa siku ya leo ni jumba kubwa la kifahari iliopo mtaa  wa Oyster bay. Nyumba hii imeandaliwa kimaalum kujumuisha sebule kubwa, ikiwa na runinga mbalimbali ambapo ndio eneo kuu la kutizamia. Vilevile “Heineken Champions Planet” ina vyumba vingine vya michezo mbali mbali ambazo zimeekezwa  PS3, meza za foosball, pool tables na chumba kulicho andaliwa binafsi kwa wanahabari. Maandalizi haya yote ni kwa ajili ya  kuweza kuwaburudisha washindi mbali mbali wa Heineken na kuwapa kumbukumbu la maisha.


Meneja mkuu wa masoko Afrika mashariki, Bwana Krijin Jansen alisema “ Kama mshiriki wa muda mrefu  wa Ligi ya Mabingwa la UEFA, Heineken inaelewa kuwa msisimko uliopo katika mashindano haya unahitaji mambo mbali mbali ya kuwachangamsha wateja wao. Kwa ushirikiano mkubwa waliotuonyesha  “Heineken Champions Planet” imetekeleza miundo mbinu hii ya kipekee ili kuwaigiza mashabiki wake kwa njia thamani.



Kutokana na umaarufu wa Heineken kote duniani, bidhaa hii imezindua njia ya  kuwashirikisha wateja katika sehemu chaguliwa za usiku nafasi ya kufuraiya mashindano ya Ligi ya Mabingwa la UEFA msimu wa 2011/12 hadi mwishoni 19 Mei katika “Heineken Champions Planet”.

No comments: