Mama mzazi wa msanii wa filamu anayehusishwa na kifo cha nyota wa filamu nchini Tanzania, Steven Kanumba (28), Elizabeth Michael 'Lulu' amesema, jamii isimuhukumu mwanawe kuwa amemuua ' Kanumba The Great'
Lucrecia Kalugila amesema, wakati Kanumba na Lulu(18) wakiwa wanagombana chumbani, walikuwa wawili tu, hivyo hakuna mwingine anayefahamu kilichotokea hivyo watu wasimuhukumu mwanawe kuwa kamuua Kanumba.
Mama huyo amesema, Kanumba ni mwanawe, na kwamba, hata yeye kifo cha msanii huyo kimemsikitisha na kwamba, kama Kanumba angekuwa hai leo, angesema namna walivyokuwa wanashirikiana.
Ametaka watu waache kuegemea upande mmoja kwenye tuhuma zinazomkabili Lulu, wasubiri sheria ichukue mkondo wake.
Amempa pole mama Kanumba, na kumshauri asiyafuate yanayosemwa mitaani kuhusu kifo cha Kanumba.
Mama Lulu amewaomba wanasheria wajitokeze kumtetea binti yake ili haki itendeke.
Lulu yupo rumande tangu Jumamosi, akihusishwa na kifo cha Kanumba, na kwa mujibu wa Polisi, atapandishwa kizimbani kujibu mashitaka ya mauaji.
KWA MUJIBU WA MDOGO WA MAREHEMU, SETI , LULU ALIKWENDA NYUMBANI KWA KANUMBA KUKAWA NA UGOMVI, WAKAINGIA CHUMBANI.
WAKATI WAKIWA HUKO, BAADA YA MUDA, LULU ALITOKA NA KUMUITA YEYE KUMUAMBIA KANUMBA KAANGUKA.
ALIPOENDA AKAMKUTA Kanumba KAANGUKA, AKAENDA kumuita DAKTARI WA KANUMBA ALIPORUDI HAKUMKUTA LULU.
Inadaiwa kwamba, Lulu aligombana na Kanumba ambaye inasemekana alikuwa mpenzi wake baada ya kukutwa akiongea na mwanaume mwingine, kwenye simu.
Hivi karibuni Lulu alinukuliwa katika kipindi cha Mkasi kinachorushwa East Africa TV 'EATV' akisema, hana MPENZI, na aliapia kiislamu kuthibitisha kauli yake.
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Charles Kenyella alinukuliwa akisema, Kanumba alikuwa katika `ugomvi’ na LULU ambaye inasemekana kuwa alikuwa mpenzi wake.
Source: SIMULIZI BLOG
No comments:
Post a Comment