WASHIRIKI wa Dar City Centre na wale wa Ukonga watasindikiza Miss Tabata kwenye utambulisho wao ambao utafanyika siku ya Pasaka Da’ West Park, Tabata.
Mratibu wa Miss Tabata Godfrey Kalinga alisema jana kuwa washiriki kutoka vituo hivyo viwili pia watatumia fursa hiyo kujitambulisha kwa wapenzi wa urembo.
“Tumewaalika Dar City Centre na Ukonga kwa sababu washindi wao watakutana na washindi wetu kwenye mashindano ya kanda ya Ilala,” Kalinga alisema.
Kalinga alisema onyesho la Pasaka litakuwa ni shamrashamra ya kusherekea miaka 10 ya Miss Tabata amabayo itaadhimishwa kwenye fainali za Miss Tabata mwezi ujao.
Katika utambulisho huo wa Jumapili, bendi za African Stars “Twanga Pepeta” na Mashauzi Classic “Wakali wa Kujiachia” watatumbuiza kwenye onyesho litakalofanyika katika ukumbi wa Dar Wes Park, Tabata.
Bendi hizo mbili zitafanya maonyesho yao kabla ya warembo kutambulishwa na hata baada ya utambulisho zitaendelea kutoa burudani kali hadi majogo huku wapenzi wao wakisherekea sikuku ya Pasaka.
Onyesho hilo maalum imeandaliwa na Bpb Entertainment na Keen Arts chini ya udhamini wa Konyagi.
Washiriki wa Miss Tabata wanaendelea na mazoezi katika ukumbi wa Dar West Park, Tabata chini ya wakufunzi watatu, Beatrice Joseph, Neema Chaki na Bokilo.
Warembo hao ni Neema Saleh (18), Paulina Valentine (18), Khadija Nurdin (19), Phillos Lemi (20) na Mercy Mlay (21). Wengine ni Neema Innocent (19), Ellen Sule (22), Wikllihemina Mvungi (20), Queen Issa (20), Suzane Deodatus (19), Everline Andrew (21), Josephine Peter (20) na Jamila Omary (19).
Warembo hao wako Zaidi ya warembo 10 kutoka Tabata watafuzu kushiriki kwenye shindano la kanda ya Ilala, Miss Ilala baadaye mwaka huu.
Mrembo anayeshikilia taji la Tabata ni Faiza Ally.
Warembo wa Tabata wamekuwa wakifanya vizuri katika mashindano ya Miss Tanzania ambapo mwaka juzi Consolata Lukosi alishinda nafasi ya tatu kabla ya kutangazwa kuwa balozi wa kinywaji cha Redds. Katika shindano la mwaka juzi Juliet William pia alishinda nafasi ya tatu katika ngazi hiyo ya taifa.
No comments:
Post a Comment