Monday, April 23, 2012

MISS UTALII TANZANIA KUTANGAZA UTALII MAREKANIWarembo wawili wa Miss Utalii Tanzania 2011, watawakilisha
Tanzania katika Shindano la Dunia la Miss United Nation 2012, litakalo
fanyika July 28 huko calfonia Marekani.Shindano hilo linashirikisha
zaidi ya nchi 100 duniani kote.


Hii
itakuwa ni fulsa nyingine ya pekee kwa nchi yetu kutangaza vivutio vya
utalii wa Tanzania , huko nchini marekani na duniani kwa ujumla. Warembo
hawa pamoja na kwenda kutangaza utalii na utamaduni wa Tanzania kwa
ujumla, lakini watapeleka ujumbe mahususi kwa wamarekani na Dunia kwa
ujumla juu ya mlima kilimanajaro,Seremgeti na Ngorongoro Crater kuwa
viko tanzania na ni mali ya tanzania. Hii itasaidia kuondoa na kupambana
na propaganda za nchi nyingine kuwa vivutio hivyo vipo kwao.


Tunafanya
mpango wa
kupata matilio mbalimbali kutika mamlaka ya Hifadhi za taifa (TANAPA),
mamlaka ya bonde la ngorongoro (NCAA) na Bodi ya Taifa ya Utalii, za
mlima kilimanjaro,serengeti na ngorongoro ikiwemo machapisho
vijarida,vipeperushi, mokanda ya video,DVD na VCD zikiwa katika lugha
mbalimbali, ambavyo warembo wetu watagawa kwa washiriki wa nchi zote ,na
vyombo mbalimbali vya habari vya nchi hizo vitakavyo ambatana na
washiriki wao,pia kupitia waandaaji hao wa dunia tutagawa katika  vituo
mbalimbali vya televisheni na magazeti nchini marekani.
Aidha mchakato wa kupata wadhamini wa kugharamia safari na ushiriki huo umeanza na unaendelea vizuri.


Mariamu
Hamisi ni mshindi wa Miss Utalii Dodoma 2011 na mshindi wa taifa wa
tuzo ya Miss Utalii tanzania 2011 - Gender,wakati Evamary Gamba ni
mshindi wa Miss Utalii tanzania Kilimanjaro 2011 na mshindi wa Taifa wa
tuzo
ya Miss Utalii Tanzania 2011 - Mount Kilimanjaro. Matarajio ya kutwaa
taji ni makubwa kutokana na ukweli kuwa washiriki wetu wanakidhi matakwa
na kanuni za kushiriki na kushinda taji la Miss United Nation World.


kabla
ya kuondoka warembo hawa watafanya ziara za mafunzo kati hifadhi za
Kilimanjaro,Ngorongoro na Serengeti, kwani ndo ajenda na kipaumbele cha
ushiriki wetu katika mashindano hayo mwaka huu. Aidha bodi ya maandakizi
ya Miss utalii tanzania ,imepitisha kuwa washiriki wote wa Miss Utalii
tanzania katika mashindano ya kimataifa na dunia watatumia ligha ya
kiswahili ,stejini ili kukitangaza kiswahili, kama ambavyo mataifa na
washiriki wa mataifa mengine wamekuwa wakitumia lugha za nchi zao na
kushinda mataji.

No comments: