Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii(TASAF), Bw Ladislaus Mwamanga
---
Na Magreth Kinabo – MAELEZO
TANZANIA kuwa mwenyeji wa mkutano wa kimataifa wa nchi zinazotekeleza mpango wa uhaulishaji fedha kwa kaya masikini utakofanyika wilayani Bagamoyo mwaka huu, kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii(TASAF), Ladislaus Mwamanga.
Amesema haya jana wakati akifungua semina ya siku moja kuhusu kutathimini utekelezaji wa mpango wa majaribio wa uhaulishaji fedha kwa kaya masikini iliyofanyika kwenye hoteli ya Malaika Beach Resorts(Livingstone) Bagamoyo.
Alisema mpango huo unaotekelezwa katika halmashuri za Bagamoyo, Kibaha na Chamwino umeonyesha mafanikio makubwa hali iliyosababisha nchi nyingine kutaka kuja kujifunza, na Benki ya Dunia kutoa fedha za mwendelezo wake.
Mwamanga aliongeza kuwa mkutano utafanyika April 24, mwaka huu, ambapo utahusisha nchi nane. Alizitaja baadhi ya nchi hizo, ni Kenya ,Uganda, Malawi, Zambia, Nigeria, Sudan ya Kusini na wafadhili yaani Benki ya Duniana UNICEF .
Alisema washiriki hao watatembelea mpango huo na kutoa mapendekezo.
Mwamanga aliongeza kuwa mpango ulianzishwa mwaka 2008 na mpaka sasa umeonyesh mafanikio mbalimbali katika jamii.
“ Mpango huu umewezesha zaidi ya watoto 1600 kutoka katika wilaya hizo walioshindwa kwenda shule kwenda shule.” alisema Mwamanga.
Aliongeza kuwa mpango umetekelezwa baada ya kuona kuwa baadhi ya kaya zinabaki kuwa masikini na kushindwa kupeleka watoto mashuleni au kupata huduma za afya mbali nao wao kuanzisha miradi ya kusaidia jamii.
Mwamanga alisema katika mpango huo wanatoa fedha kwa masharti kwa kaya masikini lengo ni kupunguza umasikini ili kupunguza idadi ya watoto walioko mitaani.
Alisema fedha za kutekeleza mpango huo zilitolewa naBenki ya Dunia ambazo ni dola za Marekani milioni 4.5 na umehusisha vijiji 40. Pia utahusisha vijiji vingine 40, umehusisha kaya 5000 hadi sasa na walengwa walengwa 13,000.
Aidha Mwamanga alifafanua kuwa mpango unajulikana kwa jina la (TASAF III), utatekelezwa nchi nzima utaanza Juali mwaka huu ambapo tayari Benki ya Dunia imeshatoa dola za Marekani milioni 220. Mpanga huo utaekelezwa katika kipindi cha miaka 10.
Mpango huo utahusisha kaya zaidi ya 20,000 na utahusisha walengwa 50,000 na vitakuwepo vijiji 78.
Naye Mkurugenzi wa Halimashauri ya Chamwino, David Mayeji alisema mpango huo umeongeza mahudhurio mashuleni kwa asilimia 99, upatikanaji wa matibabu ,ikiwemo uhakikika wa maisha.
No comments:
Post a Comment