Monday, May 21, 2012

Profesa Muhongo: Nimekuta ‘Madudu’ Ya Kutisha TanescoWAZIRI  wa Wizara ya Nishati na Madini,  Profesa Sospeter Muhongo amemkaanga mtangulize wake akisema baadhi ya madudu aliyoyakuta katika wizara hiyo ni makubwa ambayo hawezi kuyasema hadharani.
Profesa Muhongo ni miongoni mwa Mawaziri wapywa walioteuliwa Mei 3, mwaka huu kushika wadhifa katika baraza jipya la mawaziri ambapo kabla ya uteuzi huo aliteuliwa kuwa mbunge kupitia viti maalum na Rais.
Profesa Muhongo mwenye taaluma ya Jiolojia alitoa kauli hiyo juzi, alipokuwa akizunguza na wafanyakazi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) wa mikoa ya Dar es Salaam na Pwani katika mkutano wao  uliofanyika katika viwanja vya makao makuu ya Shirika hilo jijini Dar es Salaam.
Katika mkutano huo wafanya kazi walitaja mambo kadhaa yanayolifanya  shirika hilo kushindwa kujiendesha kuwa ni pamoja na mikataba mibovu iliyoingiwa na Serikali kwa Kampuni ya kufua umeme na vitendo vya baadhi ya watendaji wizarani ambao hujihusisha na hujuma dhidi ya  shirika hilo. Soma zaidi http://www.mwananchi.co.tz
 No comments: