Saturday, May 19, 2012

Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Abdallah Kigoda Amsimamisha Kazi Mkurugenzi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Charles Ekelege.


Aliyekua Mkurugenzi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Charles Ekelege.
--
WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Dk Abdallah Kigoda ameiagiza Bodi ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kumsimamisha kazi Mkurugenzi wake Mkuu, Charles Ekelege.


Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Dk Kigoda alisema Mkurugenzi huyo wa TBS anatakiwa kusimamishwa kazi ili kupisha taratibu za kisheria ikiwamo suala la uchunguzi dhidi yake kufanyika.


“Moja ya sababu iliyomfanya Rais afanye mabadiliko ya uongozi katika wizara hii ni Shirika la TBS. Kulikuwa na mjadala mkubwa bungeni kuhusu utendaji wake. Nimewataka bodi ya shirika hilo kumsimamisha kazi mkurugenzi huyo mara moja ili kupisha utaratibu mwingine wa kisheria kuanza.”

Dk Kigoda ametoa kauli hiyo ikiwa ni mara ya kwanza kuzungumza na waandishi wa habari tangu kuteuliwa kwake na Rais Jakaya Kikwete kushika wadhifa huo baada ya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri hivi karibuni.

No comments: