Wednesday, July 13, 2011

Abbas: Mguu wagu unanitesa, nisaidieni jamani...


Abas akiwa amejipumzisha nyumbani kwao.
Na Julius Magodi
ABBAS Abdalaah (31) aliapoanza kuvimba uvimbe mdogo katika mguu wake wa kulia hakujua kuwa ulikuwa ni mwanzo wa ugonjwa ambao hatimaye ungemfanya ashindwe kutembea.Ugonjwa huo ambao mpaka sasa haujulikani, umemfanya Abbas kulala kitandni muda wote akilazimika kubebwa na watu watano kumpeleka nje kujisaidia.

Matumaini aliyokuwa nayo ya kupata tiba ya ugonjwa wake, yameanza kutoweka baada ya msamaria aliyejitokeza kumpeleka Hospitali ya Seliani mjini Arusha kushindwa kutimiza ahadi yake.

Abbas ambaye ni Mkazi wa Kijiji cha Kiru Ndogo, anasema vurugu za wananchi na wawekezaji wa Bonde la Kiru, Wilaya ya Babati mkoani Manyara, ndizo anaona zimesababisha mpaka sasa asipate msaada.

“Vurugu hizi zilizoaanza Machi mwaka huu , ndizo zilizosabisha leo niwe bado hapa sina msaada, kwani mmoja wa wawekezaji katika Bonde hili alikuwa ameaahidi kunisaidia kunipeleka hospitali ya Seliani,' anasema kwa uchungu akiwa amelala katika kitanda chake kilichopo sebuleni kwenye nyumba ndogo ya nyasi ya Bibi yake, Zuhura Abdalah.

Akisimulia historia ya ugonjwa wake huo, anasema alianza kuvimba kiumbe kidogo katika mguu wake mwaka 2005, wakati huo akiwa mchezaji mzuri wa mpira wa miguu kijiji hapo.

Anasema hakuwa na wasiwasi kwamba huo ungekuwa ugonjwa mkubwa ambao ungemfikisha hapo alipo.

Taratibu mguu ulianza kuvimba, hali ambayo ilimfanya baba yake mzazi, mzee Abdallah Juma mwaka 2008, kumpeleka Hospitali ya Hydom, Wilaya ya Mbulu ambako baada ya kumchunguza hawakuona ugonjwa, ingawa mguu ulikuwa umevimba.

“Hydom hawakuona ugonjwa, nikawauliza mbona bado mguu umevimba kwa nini hamuoni tatizo, wakanishauri nirudi nyumbani, “ anasimulia kwa uchungu kijana huyu mchangamfu.


Kupata habari yote nenda Mwananchi