Saturday, July 23, 2011

‘Amuua’ mkewe kwa kupunjwa kitoweo

MKAZI wa Isalalo wilayani Mbozi mkoani Mbeya, Amina Tulianje (18) ameuawa na mumewe kwa kukatwa shoka kichwani. Sababu ya kifo hicho ndiyo inayoonekana kushangaza, kwani inadaiwa kuwa mumewe Nemes Muyombe, alifikia hatua hiyo, baada ya kukasirishwa na kitendo cha kumpunja kitoweo. Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Advocate Nyombi, jana alithibitisha kutokea tukio hilo akisisitiza kuwa chanzo cha ugomvi ni kitoweo. Ilielezwa kwamba, katika tukio hilo, mume alitumia shoka kumkata mkewe na kukimbia huku akiliacha kichwani kwa mkewe. Kamanda Nyombi alieleza kuwa, mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Mbozi iliyoko Vwawa wakati uchunguzi na juhudi za kumsaka mtuhumiwa vikiendelea.



1 comment:

Anonymous said...

Hii ni pepo mbaya aliyetuingia watanzania, pepo wa ubinafsi. Mtu huyo atafutwe, akamatwe na apate adhabu kali ili iwe fundisho kwa wengine.