Saturday, July 23, 2011

LATEST NEWS: DANNY MWAKITELEKO AFARIKI DUNIA LEO ALFAJIRI

ALIYEKUWA Mhariri wa gazeti la Rai, ambaye pia ni Naibu Mhariri Mtendaji wa New Habari, Danny Mwakiteleko , amefariki dunia leo alfajiri katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Mwakiteleko alilazwa katika kitengo cha watu mahtuti Muhimbili baada ya ajali aliyoipata juzi usiku (jumatano) eneo la Tabata (ToT) na kukimbizwa katika Hospitali ya Amana, Ilala na baadaye Muhimbili.
Katika ajali hiyo gari alilokuwa akiendesha Mwakiteleko liligongwa na lori lenye trela, ambalo lilitoweka bila kujulikana saa nne usiku. Mwakiteleko alikuwa akitokea kazini Sinza ambako alifanya kazi hadi saa tatu usiku.

Mwakiteleko alipelekwa katika Hospitali ya Amana kwa uangalizi hadi saa 12 asubuhi, ambapo madaktari waliamua apelekwe Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Baada ya uchunguzi Muhimbili, madaktari walisema majeruhi alikuwa ameumia kichwani na kumfanya apoteze fahamu kiasi (semi-conscious) hivyo ikabidi apelekwe katika chumba cha upasuaji ambako madaktari walimhangaikia kuanzia saa sita hadi saa tisa mchana.

Jana Rais Jakaya Kikwete alienda kumuona na kuelezwa kwamba hali yake inaendelea vyema.

Hii ilikuwa siku ya mwisho ya Mkutano wa Jukwaa la Wahariri mjini Arusha, Julai 16,2011.Wengine katika picha hiyo ni Mwenyekiti Absalom Kibanda (kushoto) Salim Said Salim na Neville Meena Katibu wa Jukwaa.
Latest News Tz inawapa pole wadau wote na pia kwa familia ya Marehemu. 
Gari aliyo pata nayo ajali


No comments: