Benki ya CRDB tawi la mbeya imetoa mkopo wa zaidi ya shilingi milioni 300 kwa wakulima wadogowadogo wa chai wa wilaya ya Rungwe ili waongeze uzalishaji wa zao hilo.
Hayo yamebainika wakati wa uzinduzi wa ofisi ya chama cha akiba na mikopo SACOSS cha wakulima hao.
Kaimu meneja wa benki hiyo JOHNSON MWANSOJO amesema kuwa mkopo huo utaiwezesha SACOSS hiyo kutoa huduma za kibenki.
Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika kata ya Kandete mwakaleli MWANSOJO amesema mkopo huo utanufaisha wakulima wazao wapatao elfu 15.
MWANSOJO amesema kuwa lengo la kuanzishwa kwa tawi hilo ni kuwajengea uwezo wakulima kupata fedha zao za malipo ya mazao ya kilimo na kuwaepusha kutembea umbali mrefu kutafuta malipo hayo.
Amesema hiyo ni mikakati ya CRDB kuhakikisha inawajengea uwezo wakulima na kujikita zaidi katika uzalishaji wa chai na kuwawezesha kupata mikopo kwa uraisi kupitia SACOSS yao ili kujikwamua na umaskini
Na mwandishi wetu Mbeya
No comments:
Post a Comment