RAIS Jakaya Kikwete ameridhia idadi ya maofisa katika ziara zake za nje ipunguzwe ikiwa ni hatua ya kupunguza gharama. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe aliliambia Bunge mwishoni mwa wiki wakati akijibu hoja ya kambi ya upinzani iliyoendelea kutaka safari za nje kwa viongozi zipunguzwe. Membe alisema katika safari ya hivi karibuni ya Rais Kikwete nchini Shelisheli, idadi ya maofisa alioongozana nao ilikuwa 34 na kwa safari ya Afrika Kusini ilikuwa 34.
No comments:
Post a Comment