Wednesday, July 13, 2011

BENKI YA NBC YATOA TUZO YA HESHIMA KWA WAFANYAKAZI WAKE JIJINI DAR ES SALAAM

Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya NBC, Lawrence Mafuru akimkabidhi Bi. Anna Leon Mushi tuzo ya ‘Mkurugenzi Mtendaji’ katika hafla ya kila mwaka ambayo benki hiyo ilikabidhi tuzo mbalimbali kwa wafanyakazi wake bora maarufu kama ‘Heshima Awards’ jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya NBC wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Lawrence Mafuru (wa sita kushoto mstari wa nyuma) katika hafla ya kila mwaka ambayo benki hiyo hukabidhi tuzo mbalimbali kwa wafanyakazi wake bora maarufu kama ‘Heshima Awards’ jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
.....................................
NA MWANDISHI WETU

JUMLA ya wafanyakazi kumi na tatu wa Benkiya NBC Tanzania wamekabidhiwa zawadi mbalimbali kutokana na utendaji kazi waouliotukuka katika sherehe zilizofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
Kwa kawaida kila mwaka NBC hutoa tuzo katika tukiolijulikanalo kama ‘Heshima Awards’ ikiwa ni kama ishara ya Menejimenti ya NBCkuridhishwa na utendaji kazi wa wafanyakazi wa benki hiyo kwa mwaka wa fedhauliopita.
Akizungumza wakati wa hafla ya kuwatunukiawafanyakazi hao, Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Lawrence Mafuru alisema kuwa hiyoilikuwa ni mara ya nne kwa wafanyakazi kutunukiwa Heshima Awards.
“Kila mwaka huwa tunaangalia vipengele vinne katikatuzo zetu navyo ni Jamii; Wateja; Uongozi/Wafanyakazi na Fedha/Wanahisa,” alisemaMafuru.
Washindi walikabidhiwa vyeti, fedhataslimu huku majina yao yakipelekwa kushindanishwa kwenye tuzo za benki mama yaNBC, ABSA.

“Wafayakaziwote wa NBC walishiriki kuwachagua washindi hawa kwa kujaza fomu maalumu nakutoa sababu za kuwachagua wastakaoshindania tuzo za fedha, shaba na dhahabu. Kishafomu hizo hukabidhiwa kwenye Kamati Maalumu ya Heshima Awards kwa shughuli zakukamilisha zoezi lenyewe,” alisema Mafuru.

Washindi wa mwaka huu waliopata tuzo za dhahabu ni Rajab Maalim( tawila Zanzibar), Salma Yatera(tawi la Moshi), Jacqueline Sindano(tawi la Corporate,Dar-es-Salaam), na Margareth Touwa(tawi la Mwanza) na zawadi kubwa kabisa ya hafla hiyo ya mshindi wa MD iliangukia kwa Anna Leon Moshi kutoka tawi la NBC Babati.

“Hakika tukio hili linahamasisha sana. Linaonyesha jinsi uongozi wa NBCunavyowajali wafanyakazi wake,” mmoja wa waalikwa alisema baada ya washindikutunukiwa.
Washindi siku zote ni wale waliofanya jambo kubwalitakalowashawishi wajumbe wa kamati na wafanyakazi wote wa benki kuamini kuwamuhusika anapaswa kuzawadiwa.
Miongoni mwa mifano iliyowazi ni tukio la Desembamwaka jana wakati Luciana Kipiko alipopokea hundi yenye thamani ya Sh 46,750,000iliyochukulewa kwenye Tawi la Corporate Dar es Salaam na kupelekwa tawi la Dodoma.
Baada ya kuishitukia, Luciana aliituma kwa fax Dar es Salaam iliithibitishwe na hata ilipothibitishwa bado Luciana aliitilia shaka na kuamuakumpigia simu Meneja wa Corpaorate, na ikagundulika kuwa ilikuwa imeghushiwa.
“Kitu kama hicho kilitokea kwa mfanyakazi wa Tawi laMwanza, Margareth Touwa aliyeishitukia hundi ya Sh 221,000,000 iliyopelekwa na Mnada Enterprises Machi mwaka jana na kesi bado ikomahakamani.
“Hivyo ni muhimu kamasi lazima kwa NBC kuthamini michango na kujitolea kwa dhati kunakofanywa nawafanyakazi wa aina hii,” alisema MD.

Ends