Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitia saini katika kitabu cha maombolezo ya marehemu Profesa, Samuel Mushi, aliyefariki wiki iliyopita jijini Dar es Salaam. Shughuli za maziko na kuaga mwili wa marehemu zilifanyika kwenye Ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu cha Dar es Salaam leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima ya mwisho mbele ya jeneza lenye mwili ya Marehemu Profesa Samuel Mushi, wakati alipofika katika shughuli ya kuaga iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, pamoja na baadhi ya viongozi wakiwa katika shughuli ya mazishi na kuaga mwili wa marehemu Profesa Samuel Mushi, iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu cha Dar es Salaam leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifurahia jambo na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, nje ya ukumbi wa Nkurumah baada ya kuaga mwili ya marehemu Profesa Samuel Mushi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Waziri Mstaafu, Fredrick Sumaye, nje ya ukumbi wa Nkurumah baada ya kuaga mwili ya marehemu Profesa Samuel Mushi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, leo. Katikati ni Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwafariji wanafamilia ya marehemu Profesa Samuel Mushi, alipofika kuaga mwili katika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, leo
Baadhi ya wanafamilia ya marehemu Profesa Mushi, na ndugu jamaa na marafiki, wakiwa katika shughuli za mazishi na kuaga mwili wa marehemu Profesa Samuel Mushi, iliyofanyika leo, kwenye ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Picha na Muhidin Sufiani-OMR
No comments:
Post a Comment