Monday, July 18, 2011

FAMILIA NNE ZA FFU SINGIDA ZANUSURIKA KUUNGUA KWA MOTO

Familia nne za askari Polisi wa kikosi cha kutuliza ghasia FFU mkoani Singida, zimesurika kufa, baada ya nyumba yao kuteketea kwa moto uliosababishwa na mshumaa uliokuwa umewashwa. Kamanda wa polisi mkoani humo Bi Celina Kaluba amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo, saa tisa alfajiri kwenye kambi ya kikosi cha FFU, iliyopo eneo la Manguanjuki, nje kidogo ya mji wa Singida.
Amesema moto huo umesabaisha vifaa vyote vya ndani vya familia hizo, vyenye thamani ya zaidi ya Sh.Milioni nane na fedha taslimu Shilingi laki nne, kuteketea. Bi Kaluba amesema chanzo cha ajali ya moto huo hakijafahamika mpaka sasa.
Kwa upande wa Majirani katika eneo waliozungumza na kituo hiki wameeleza kwamba moto huo ulisababishwa na mshumaa uliowashwa usiku na mmoja wa askari katika nyumba hizo,lakini alipozidiwa na usingizi, moto ulishika kwenye godoro, na kusambaa kwenye vyumba vingine na kuteketeza mali zilizokuwepo.

1 comment:

Wilabrd said...

Hii ni kwa sababu ya ukosefu wa umeme. Umeme ungekuwepo wasingewasha mshumaa. Wizara ya nishati iwafidie.