Saturday, July 23, 2011

KUTOKANA NA VURUGU YA MALAWI WATANZANIA WAFANYIWA JITIHADA ZA KURUDISHWA

Kutokana na vurugu zinazoendelea Nchini Malawi mkuu wa mkoa wa Mbeya John Mwakipesile amesema Serikali mkoani hapa inaendelea na kuwasiliana na ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini humo ili kuwarejesha watanzania nyumbani.

Akiongea na Bomba Fm kwa njia ya simu Mwakipesile amesema taarifa za vurugu zimemfikia na kwamba hatua inayoendelea hivi sasa ni namna mbavyo watanzania wanaweza kurejeshwa nchini mwao wakiwa katika hali ya usalama.

Habari tulizo zipata hivi punde zinadai kuwa Wataalamu wa uchumi nchini Malawi wamesema kutokana na matukio ya maandamano nchini humo, serikali inapaswa kufikiria upya sera yake ya kushusha thamani ya sarafu ya nchi hiyo.

Wasiwasi wa kiuchumi pamoja na kidemokrasia dhidi ya serikali ya rais Bingu Wa Mutharika huku kukiwa na upungufu mkubwa wa mafuta uliozusha ghasia nchi nzima siku ya Jumatano wakati waandamanaji walipotoa wito kwa Mutharika kujiuzulu.

Watu walipora maduka na kuchoma mali katika mapambano kati ya raia ya polisi nchini humo ambapo uporaji uliendelea katika baadhi ya maeneo ya Lilongwe na Blantaya jana Alhamis asubuhi na magari ya jeshi yameonekana yakifanya doria katika mitaa wakati jeshi liliitwa kuzima ghasia hizo.

Habari na mwandishi wetu wa Mbeya

No comments: