Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Aggrey Mwanri akijibu swali la Mbunge wa Biharamulo Magharibi Dkt. Anthony Mbassa (hayupo pichani) kuhusu Serikali kugawa maeneo mapya katika wilaya hiyo wakati wa kipindi cha Maswali na majibu Bungeni leo mjini Dodoma.
Waziri Mkuu Mizengo Kayanza Pinda kulia akimsikiliza waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Prof. Jummanne Maghembe (kushoto) wakati wa kipindi cha maswali na majibu katika kikao cha Bunge la bajeti kinachoendelea mjini Dodoma.
Mbunge wa Same Mashariki Anna Kilango Malecela akichangia bajeti ya wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika kuhusu umuhimu wa wakulima kuuza mazao yao nje ya nchi.
Mbunge wa Jimbo la Nyang’hwale (CCM) (kushoto) Hussein Nassoro Amar akisalimiana na Patrick Grones (kulia) ambaye ni Mwalimu wa Shule ya Sekondari St. Ignatius Collage ya Mjini London Nchini Uingereza nje ya viwanja vya Bunge mjini Dodoma. Wanafunzi hao wako nchini kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali ambapo leo wamepata fursa ya kutembelea Bunge.
Mbunge wa Mbeya Mjini (CHADEMA) Joseph Mbilinyi akiuliza swali kuhusu umuhimu wa Serikali kukichukua Kiwanda cha Zana za Kilimo Mbeya ili kukidhi malengo ya uanzishwaji wake kwenda sambamba na mkakati wa kilimo kwanza pamoja na kuongeza ajira kwa wananchi wa mkoa huo.
Waziri wa Katiba na Sheria Celina Kombani (kulia) na Mbunge wa viti Maalum (CHADEMA) Suzan Kiwanga (kushoto) wakimsikiliza Mbunge wa Maswa Magharibi (CHADEMA) John Shibuda nje ya viwanja vya Bunge mjini Dodoma leo mara baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu.
No comments:
Post a Comment