Wednesday, July 13, 2011

Mfalme wa Ashanti Otumfuo Osei Tutu II Atembelea Zanzibar Nakukutana na Makamu Wa Kwanza Wa Rais Maalim Seif Sharrif na Makamu Wa Pili Wa Rais Balozi Seif idd

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Mwinyihaji Makame akimsalimia Mfalme wa Ashanti Otumfuo Osei Tutu II, alipowasili Uwanja wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume kwa ziara ya siku moja Zinzibar.
MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad,akizungumza na mgeni wake Mfalme wa Ashanti Otumfuo Osei Tutu II, alipofika Ofisini kwake kwa mazungumzo.
MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maali Seif Sharif Hamad akipokea zawadi kutoka kwa Msaidi wa Mfalme wa Ashanti, alipofika Ofisi kwa Makamu kwa mazungumzo.
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa mgeni wake Mfalme wa Ashanti Otumfuo Osei Tutu II, alipofika Ofisini kwake kwa mazungumzo Vuga.
MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad na Mfalme wa Ashanti Otumfuo Osei Tutu II, wakiwa katika picha ya pamoja nje ya Ofisi ya Makamu Migombani.
MFALME wa Ashanti Otumfuo Osei Tutu II, akipata maelezo ya mkarafuu katika shamba la kizimbani akiwa katika ziara yake Zanzibar, akiwa na Mwenyeki wake Dk. Mwinyihaji Makame.
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Mwinyihaji Makame akitowa maelezo ya miti ya Viungo katika shamba la Kizimbani.