Friday, July 29, 2011

Msanii kizimbani, adaiwa kunajisi

MSANII wa uchoraji Geofrey Liponda (18) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala mkoani Dar es Salaam akikabiliwa na mashitaka ya kumnajisi mtoto wa miaka 13. Liponda alifikishwa mahakamani hapo jana na kusomewa mashitaka yake mbele ya Hakimu Mkazi, Janeth Kaluyenda. Wakili wa Serikali Anunciatha Leopold alidai mbele ya Hakimu Janeth Kaluyenda kuwa, Julai 19, mwaka huu, katika eneo la Kiwalani Minazi Mirefu, Liponda alimuingilia kimwili mtoto huyo. Mshitakiwa alikana mashitaka na kurudishwa rumande hadi Agosti 11, mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.

Chanzo: Habari Leo

No comments: