Saturday, July 23, 2011

Latest News: Mwandishi Simon Mkina Naye Amepata Ajali

Taarifa hii kutoka mtandao wa Wanabidii
Ninawajulisha kwamba Simon Mkina mwanahabari na mmoja wa viongozi na waratibu wa mtandao huu amepata ajali baada ya gari lake kugonga nguzo akitoka kazini kuelekea nyumbani. Kwa sasa amelazwa kwenye hospitali ya IMTU iliyopo maeneo ya Mbezi Beach ukiwa unaelekea Tegeta.
Naombeni wanabidii mlio karibu mkamcheki pale kwa msaada zaidi. Taarifa za awali zinasema ameumia zaidi eneo la kifuani na kwa sasa madaktari wanajitahidi kumchunguza maeneo mengine ya mwili kwa vipimo.
Nimepata taarifa hizi niko safarini Tanga. Washirika wa karibu hapo Dar tunaombeni msaada wa kumfuatilia huyu mpiganaji wa jukwaa letu.
Joachim Mushi


No comments: