tuzo aliyotunukiwa Naibu Spika Mhe. Job Ndugai
Mwakilishi wa Chama cha Wabunge wanawake wa Jumuiya ya Madola Afrika (CPA) katika Mkutano Mkuu wa 57 wa CPA Dunia Mhe. Beatrice Shelukindo akipokea tuzo kwa niaba ya Naibu Spika Mhe. Job Ndugai kutoka kwa mwenyekiti wa CPA anayemaliza mda wake Mhe. Mohamed Shafie Apdal kutoka Malaysia ambayo Mhe Ndugai amezawadiwa kwa kuitumikia kamati tendaji ya CPA kwa mda wa Miaka mitatu. Mhe. ndugai amekuwa mjumbe wa Kamati kuu tendaji ya CPA tangu mwaka 2008 ambapo mda wake umekwisha mwaka huu. Mkutano Mkuu wa CPA umemalizika Jana jijini London Uingereza.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akimwaga rasmi Naibu Spika wa Bunge la Uingerza Mhe. Nigel Evance mara baada ya kumalizika rasmi kwa mkutano wa 57 wa CPA ambao ulifanyika London Uingereza kwa kukutanisha Maspika, Maseneta na Wabunge zaidi ya 700 kutoka nchi 52 za Jumuiya ya Madola kujadili maswala mbalimbali yahusuyo uendeshaji wa Mabunge katika mabunge wanachama wa Jumuiya hiyo .
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akifurahia jambo na Spika wa Bunge la Malawi Mhe. Henry Chimuntu Banda mara baada ya kumalizika rasmi kwa mkutano wa 57 wa CPA ambao ulifanyika London Uingereza kwa kukutanisha Maspika, Maseneta na Wabunge zaidi ya 700 kutoka nchi 52 za Jumuiya ya Madola kujadili maswala mbalimbali yahusuyo uendeshaji wa Mabunge katika mabunge wanachama wa Jumuiya hiyo .
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda (Mb) akiwa katika picha ya Pamoja na Naibu Spika wa Bunge la Uingerza Mhe. Nigel Evance (Mb) (Mwenye tai) pamoja na Mwenyekiti Mpya wa CPA Mhe Sir Alan Heselhurst (Mb) mara baada ya kumalizika rasmi kwa mkutano wa 57 wa CPA ambao ulifanyika London Uingereza kwa kukutanisha Maspika, Maseneta na Wabunge zaidi ya 700 kutoka nchi 52 za Jumuiya ya Madola kujadili maswala mbalimbali yahusuyo uendeshaji wa Mabunge katika mabunge wanachama wa Jumuiya hiyo . Wengine katika picha ni Ujumbe wa Tanzania ulioambatana na Mhe. Spika katika Mkutano huo na Katibu Mkuu wa CP Dkt William Shija
( Nyuma ya Spika)
Picha na Owen Mwandumbya wa Bunge.
No comments:
Post a Comment