Saturday, July 23, 2011

NAPE ADAI KUNASA NYARAKA ZA UCHOCHEZI ZINAZOSAMBAZWA NA CHADEMA

NA MWANDISHI WETU, MOSHI
KATIBU wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amedai kuzinasa nyaraka za  zinazosambazwa na CHADEMA nchi  nzima kuchochea  maandamano na kuzuia wananchi kuchangia shughuli za maendeleo nchi nzima.
Akizungunza katika mkutano wa hadhara uliofanyika jana kwenye Stendi  Kuu ya mabasi mjini Moshi, Nape alisema, nyaraka alizonasa ni pamoja na baruza yenye kumbukumbu namba CDM/DSM/HU/Vol 040/2011 ya Julai 20, 2011, ambayo CHADEMA imewasambazia wenyeviti wa chama hicho kila mkoa  kuchoandaa maandamano nchi nzima baada ya kikao cha Bunge la bajeti.
 Kwa mujibu wa Nape barua hiyo ambayo imesainiwa na  Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CAHDEMA,  Erasto Tumbo  barua hiyo inashinikiza wenyeviti hao  kutekeleza maamuzi ya Kamati Kuu ya chama hicho kuandaa maandamano  hayo ili kuiwaibisha serikali kwa madai kwamba imeshindwa kutekeleza majukumu ya kuwaletea maendeleo wananchi.
“Ni  jukumu lako Mwenyekiti na makatibu wa majimbo katika mikoa kuanza kuhamasisha wananchi na kupanga wafuasi kikamilifu kwani harakati za awamu hii ni ndefu sana baada ya vikao vya bunge”,  Nape alinukuu sehemu ya barua hiyo ambayo aliionyesha  katika mkutano huu.
Alisema barua nyingine ni yenye kumbukumbu namba  CDM/DSM/ Vol. 138/2011 ya Juni 30,2011 ambayo pia imesainiwa na Tumbo iliyosambazwa kwa Makatibu wa Majimbo kutakiwa kutekeleza agizo la Kaatibu Mkuu wa CHADEMA Wilborod Slaa kuhamasisha wananchi wagome shughuli za maendeleo.
Barua hiyo ambayo  Nape aliionyesha mkutanoni ina kichwa ‘ Utekelezaji wa agizo la Katibu Mkuu kuhamasisha wananchi wagome kuchangia shughuli za maendeleo”.
“”Unatakiwa kutekeleza agizo la Katibu Mkuu (Wilbrod Slaa) kuhamasisha wananchi wagome kuchangia shughuli za maendeleo …Tayari mhe. Katibu Mkuu keshafanya hivyo majimbo kadhaa hasa kule Songea ambapo muzimu huo unaitafuna serikali ya CCM na wabunge”  Nape alikariri sehemu ya barua hiyo yenye ukurasa mmoja.
Nape aliwataka wananchi kote nchini kukaataa kuingia kwenye mtego wa CHADEMA ambao alisema wanauandaa kwa sababu hawana uchungu na nchi, wanataka  wananchi wache kuchangia maendeleo na badala yake watumbukie katika maandamano ambayo hayatawapa faida yoyote badala ya kuwaongezea dhiki. 
Alisema, wakati Chadema watataka kuhamaisha  wananchi kutochangia shughuli za maendeleo ,  wananchi wenyewe ni mashahidi kwamba yapo mafanikio mengi ambayo yamepatikana katika maeneo mbalimbali nchini  kutokana na uchangiaji. 
Nape alitaja moja ya mafanikio yaliyopatikana kutokana na uchangiaji kuwa ni ujenzi wa shule za sekondari za Kata, ambazo kutokana  na kujengwa kwake sasa waatoto wengi wamepata fursa ya kwenda shule. 
Kabla ya kuhutubia mkutano huo, Nape alifungua shina la wana-CCM wapya lililoundwa na wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Tumaini cha Kumbukumbu ya Mtakatifu Stephano (SIMCO) kilichopo Mwika, Moshi Vijijini ambapo jumla ya wanachama  wapya 108 wa CCM walikabidhiwa kadi. 
Akizungumza naa wasomi hao katika  kutano uliofanyika katika ukumbi wa  King Size,  Himo, Nape aliwataka wanafunzi kutambua kwamba siasaa siyo ajira bali ni tunu ambayo humtokea mtu baadaye  baada ya kufanya maandalizi katika mambo mengine.
Aliwataka kutoingia katika siasa kwa lengo la kuifanya ndiyo ajira yao kwa kuwa kufanya hivyo wakati bado wapo masomoni haatafanikiwa vyote kwa kuwa ni rahisi kuanguka kimasomo mtu atakapogeuza siasa kuwa mradi. 
Nape aliwataka wanafunzi waliofungua tawi  kuwa chachu ya mabadiliko ndani ya chama na sikwa lengo la kutafuta vyeo kama ambavyo wengi wanadhani. 
Mwisho.

1 comment:

Anonymous said...

habar ipo nusu sana, nimeshuhudia mwenyewe, uchache wa watu, mwisho alivyözomea. Ripoti haijabalance, na ndio tatzo la waandshi ndio hlo, kutokubalance habar.