Wednesday, July 27, 2011

WABUNGE WASUTANA DODOMA LEO

Mbunge wa Ludewa (CCM) Deo Filikunjombe (kushoto) akisutwa nje ya ukumbi wa Bunge na wabunge wa upinzani baada ya Filikunjombe kumwambia Ezekia Wenje Mbunge wa Nyamagana (CHADEMA) (hayupo pichani) alikosa ustaarabu kwa kutokumtii Mwenyekiti wa kikao cha Bunge cha leo Mbunge wa Dole (CCM) Silvester Mabumba pale alipomwambia akae chini na kutokutoa hoja ya dharula kuhusu samaki wa sumu kutoka Japan.
Pamoja na kusepa lakini Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA), Suzan Kiwanga (aliyevaa kitenge) aliendelea kula nae sahani moja.
Pamoja na kusepa lakini Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA), Suzan Kiwanga (aliyevaa kitenge) aliendelea kula nae sahani moja.
Mbunge wa Nyamagana (CHADEMA) Ezekia Wenje (aliyevaa suti ya rangi ya maziwa) akitolewa nje ya ukumbi wa Bunge na Askari Polisi wa Bunge baada ya kutokumtii Mwenyekiti wa kikao cha Bunge cha leo Mbunge wa Dole (CCM) Silvester Mabumba pale alipomwambia akae chini na kutokutoa hoja ya dharula kuhusu samaki wa sumu kutoka Japan.

PICHA/ANNA NKINDA WA MAELEZO


Bunge la Jamhuri ya Muungano limelazimika kumtoa nje ya Ukumbi wa Bunge Mbunge wa Jimbo la NYAMAGANA, EZEKIA DIBOGO WENJE kufuatia mabishano kati yake na Mwenyekiti wa Bunge SYLVESTER MASELE MABUMBA wakati wa kikao mara baada ya kipindi cha maswali na majibu kumalizika.

Hatua hiyo imekuja wakati Bunge likiwa kwenye kikao chake cha 34 cha Mkutano wa NNE ikiwa ni adhabu ya kwanza kuchukuliwa na Bunge la kumi linaloendelea na vikao vyake mjini Dodoma.

Baada ya mtafaruku wa kisheria baina ya Mbunge wa Jimbo la Singida Kusini TUNDU LISU, MOSES MACHALI wa Jimbo la KASULU MJINI kuhusu miongozo, zamu sasa ikawa baina ya Mbunge wa NYAMAGANA, EZEKIA DIBOGO WENJE akiomba Bunge liahirishe shughuli za leo ili aweze kutoa hoja ya dharura na kujadiliwa na Bunge.

No comments: