Tuesday, July 12, 2011

WITO KWA WASANII SAUTI ZA BUSARA 2012


Je muziki wako ni wa laivu?

Je muziki wako umeungana na Afrika?

Je umevutiwa kupiga muziki mwezi ujao wa Februari katika Afrika Mashariki?

Kama unaweza kujibu ndio, ndio, ndio - basi endelea kusoma...


Muziki wa Afrika – chini ya mawingu ya Afrika. Sauti za Busara ni tamasha linalo fanyika kila mwaka hapa Afrika ya mashariki na limekuwa lijulikana kama “Tamasha rafiki zaidi duniani”. Tamasha la nane la Sauti za Busara litafanyika tarehe 8 mpaka 1 2 Februari 2012. Likija pamoja na
  • 400 Wanamuziki : Hivyo ni vikundi arobaini, ishirini vikitoka hapa hapa Tanzania, na ishirini kutoka sehemu nyingine za Afrika. Vikundi vya mijini, mashamba, vikundi vinavyotumia vyombo vya umeme, vilivyoanzishwa na vikundi chipukizi.
  • Maandamano ya Ufunguzi : Maandamano ya tapitayo barabara kuu katika siku ya ufunguzi, ikiwemo ngoma ya beni, ngoma za kienyeji, kikundi cha wanawake cha mwanandege, sarakasi, na viburudisho vingi vya kushangaza. Angalia Maandamano ya Ufunguzi.
  • Swahili Encounters : Siku nne ambazo wasanii hushirikiana, wenyeji walioalikwa, wanamuziki wanaotembelea tamasha hupata muda wa kuzitafsiri nyimbo za kiswahili na kuziwasilisha jukwaani.
  • Angalia Swahili Encounters.
  • Semina za Mafunzo : Kuwajenga wasanii, viongozi, waandishi wa habari, watengeneza filamu, na mafundi wa vipaza sauti na taa kuwa na ujuzi endelevu kutoka hapa Afrika ya mashariki.
  • Waanzilishi wa Sanaa : Makongamano ya kila siku yanayowakutanisha wataalamu wa sanaa wa hapa nyambani na wakigeni.
  • Filamu za Muziki wa Kiafrika : Filamu za muziki za kumbukumbu, filamu ndogo ndogo za muziki, video, na filamu za burudani za laivu.
  • Busara Xtra : Wakati wa tamasha Kisiwa cha Zanzibar hurindima na matukio tofauti. Ngoma za kienyeji, ngoma za kudensi, shoo za kiana, mashindano ya ngalawa, viburudisho vya baada ya pati, na burudani za taarabu asilia hupangwa na wenyeji.