| Leo mchana Wizara ya Nishati na Madini, jijini Dar es Salaam, kulitokea hali ya sintofahamu iliyodumu kwa takribani dakika 25 hivi. Ni wakati baadhi ya waandishi wakiwa na baadhi ya wamiliki wa makampuni ya kuuza mafuta waliokuwa wakielekea ghorofa ya tano kwenye mkutano wa kujadili hali ya mgomo wa baadhi ya vituo vya mafuta, kukwama kwenye lifti. Hali hiyo ilizua wasiwasi mkubwa. Baada ya kupatwa na dhahama hiyo ilipigwa simu ya dharura na ilichukua muda mrefu kuhudumiwa, hali ilyopelekea wasiwasi mkubwa kwa tulikuwemo kwenye lifti hiyo. Joto kali na kukosa hewa ya kutosha kulitishia uhai wetu. Mdau wenu Victor Makinda, nilikuwepo ndani ya lifti hiyo na nilikuwa wa kwanza kutoka pale ulipofunguliwa mlango wa lifti hiyo na mhudumu aliyefika kwa kuchelewa na ndipo nilipoweza kupiga picha hizi. |
No comments:
Post a Comment