Thursday, August 18, 2011

AJALI YAUA WATU WATANO MORO USIKU WA KUAMKIA JANA


MKOA wa Morogoro unaendelea kuandamwa na mzimu wa ajali,ambapo usiku wa kuamkia leo ajali nyingine mbaya iliyoyahusisha maroli mawili, Scania lenye namba za usajili T 830 BFZ na Canter yenye namba za usajili T 845 BSD kutokea maeneo ya Fulwe, Mikese mkoani hapa baada ya maroli hayo kugongana uso kwa uso na kusababisha watu watano kufariki dunia papohapo na majeruhi mmoja ambaye amelazwa katika hospitali ya mkoa wa Morogoro.

Mwandishi wetu alifika eneo la tukio na kuyakuta maroli hayo yakiwa yameharibika vibaya huku madereva wote wakiwa ni miongoni mwa watu waliopoteza maisha.

Zifuatzao ni picha zaidi za tukio hilo:
NA DUNSTAN SHEKIDELE, MOROGORO
Habari kwa hisani ya Global Publishers 

No comments: