Thursday, August 18, 2011

Breaking Nuuuz...... Halmashauri kuu ya Mbomipa yavunjwa kwa ufisadi wa shilingi milioni 50 za mkataba wa uwindaji


Na  Francis Godwin,Iringa

WAKATI mjadala  wa  wizara ya Maliasili na utaliiukiendelea kutikisa kikao cha bajeti cha bunge la jamhuri ya muungano  wa Tanzania mjini Dodoma , serikali ya wilaya ya Iringa imeingilia kati sakata la ufisadi wa mkataba  feki wa uwindaji katika mradi  wa  wa Hifadhi ya Mali Hai (Mbomipa) unaoundwa na vijiji 22 vya Tarafa za Idodi na Pawaga, vinavyozunguka Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, wilayani Iringa  kwa  kuivunja Halmashauri  kuu ya Mbomipa baada ya  kudaiwa  kuhusika na ufisadi wa shilingi milioni 50 katika maradi  huo.

Katibu  bodi ya Wadhamini wa Mbomipa, Michael Filiakosi akikili  kuvunjwa  kwa Halmashauri  hiyo  na kudai  kuwa uwindaji haramu  unaofanywa katika eneo la Mkupula ambalo lilikuwa chini ya kampuni ya Marera ndio umepelekea hata  wanyama katika eneo hilo kupungua  huku viongozi  wa Halmashauri kuu  wakiendelea  kusaini mikataba feki.

Filiakosi alisema mradi  huo ambao upo kwa ajili ya  kuendeleza shughuli za utalii , upigaji wa picha wa wanyama waliomo kwenye hifadhi hiyo na uwindaji umeendelea kupoteza mwelekeo  wake

Alisema baadhi ya watu waliokuwa wamenunua vitalu katika hifadhi hiyo, wamevitumia vibaya baada hasa kwa vitendo vya kuwaua wanyama kiholela na kusababisha idadi yao kupungua.

Katibu huyo wa Mbomipa, vitendo hivyo vimesababisha kupungua kwa idadi ya watalii waliokuwa wakitembelea hifadhi hiyo kubwa nchini .

Alisema  wanyama kama Nyati ,simba, tembo na swala  sasa wamepungua kwa kiwango kikubwa katika hifadhi ya Ruaha na hii imesababishwa na uwindaji haramu unaotetewa na Halmashauri kuu ya Mbomipa.

Alisema  kuwa mbali ya uwindaji haramu ila bado hata  malengo ya Mradi  huo ulianzishwa kwa ajili ya  kuwanufaisha  wananchi  wa vijiji 22 vya mradi  huo ,bado yametoweka na badala yake kuwa mradi  wenye  kuwanufaisha  zaidi viongozi wachache wa Halmashauri kuu ya Mbomipa.

Alisema  kuwa katika  kikao cha kamati kuu ya Mbomipa na bodi ya wadhamini  kilichofanyika juni 25 mwaka huu katika ukumbi wa Lutherani Centre pamoja  na mambo mengine  wajumbe  walipokea taarifa  kutoka kwa mwenyekiti  juu ya wizara kumaliza mgogoro  huo pamoja na kuwasilisha hati za maelewano kati ya bodi na kampuni ya Marera , mkataba wa uwekezaji kati ya kampuni ya Marera na Mbomipa mkakata ambao umeonekana  kuwa ni feki baada ya uchunguzi .

Hata  hivyo katika hati  hizo  mjadala mkali ulipata  kuibuka baada ya  wajumbe  kukana kukaa na kampuni ya Marera Safari  Lodge  na  kufikia makubaliano hayo kutokana na kutokuwepo kwa hati iliyosainiwa na bodi ya  wadhamini wala bodi haijawahi kumuagiza mtu yeyote  aingie makubaliano ya aina hiyo  kwa niaba na bodi .

Huku juu ya mkataba  huo feki mkabata  huo ni  wa viongozi hao  wawili makamu mwenyekiti na katibu  wake  wa Halmashauri ya Mbomipa na sio kwa ajili ya mradi  huo wa Mbomipa ambao unataka bodi ya wadhamini  kusaini mikataba kwa niaba ya Mradi  huo wa Mbomipa na si vinginevyo.


Pia alipongeza hatua ya mkuu wa wilaya ya Iringa kepten mstaafu Aser Msangi katika kikao chake cha pamoja na bodi na Halmashauri kuu ya Mbomipa  kilichokiti wiki iliyopita  kwa uamuzi  wa kuvunja Halmashauri  hiyo baada ya   kuwepo kwa ufisadi  huo  wa  fedha kiasi cha shilingi milioni 50 ambazo hazikuingizwa katika akaunti ya Mbomipa  huku viongozi  wa Halmashauri  ya Mbomipa wakidaiwa  kuizunguka bodi ya  wadhamini na kusaini mkakata na mwekezaji  kinyume na katiba ya Mbomipa.

Mmoja kati ya  wajumbe  wa Halmashauri kuu ya Mbomipa ambaye hakupenda  kutaja  jina lake alidai  kuwa viongozi  wa Halmashauri  hiyo ambao  wameondolewa madarakani ili kupisha uchaguzi mpya   ulipangwa  kjufanyika ndani ya wiki mbili kuanzia sasa ,kuwa  viongozi hao  walikuwa   wakiendesha mradi  huo kwa maslahi yao na kuwatumia  wajumbe  wa vijiji  vya Pawaga ambavyo ni miongoni mwa vijiji jirani vya maradi huo vinavhyonufaika na mradi ili kujiwekea uhalali wa kuungwa mkono kama njia ya kuendeleza ufisadi ndani ya mradi  huo.

Hata  hivyo alisema kuwa  katibu wa Halmashauri  kuu ya Mbomipa Josephat Kisanyage  na makamu mwenyekiti  wake Mashauri Msavi    walisafiri kwa ndege  kwenda Arusha kwa mwekezaji kwa ajili ya kusaini mkataba feki ,mkataba uliopaswa kusainiwa na bodi  bila hata  wajumbe  wa Halmashauri kuu ya Mbomipa  kujulishwa  zaidi ya kupewa taarifa  baada ya kurejea kuwa  wameingia mkakaba na mwekezaji wa kampuni ya Marera.

Mjumbe  huyo kutoka Idodi anadai kuwa  wajumbe kutoka Pawaga ndio ambao  walikuwa  wakiiunga mkono mkataba  huo feki pamoja na viongozi hao  ambao  katika kikao cha Halmashauri  kuu  kilichofanyika Nzihi  viongozi hao  walipania kuivunja bodi ya  wadhamini kwa baada ya kuibua ufisadi wa shilingi milioni 50.

Alisema kuwa njama za viongozi  wa Halmashauri kuu kutaka  kuvunja bodi  hiyo  ziligonga mwamba baada ya   mwanasheria  wa wilaya  kuingilia kati na kupinga uamuzi  huo kwa madai kuwa mwenye haki ya kuvunja bodi ni msajili wa serikali  kwa mujibu wa katiba na si vinginevyo. 

Pia alisema  kuwa mbali ya hatua iliyofikiwa na mkuu  wa wilaya ya kuivunja Halmashauri  hiyo bado  wizara ya maliasili iliifutia kibali kampuni ya Marera kuendelea  kufanya kazi ya uwindaji katika mradi  huo wa Mbomipa.

Aidha alisema katika kikao hicho kilichohudhuliwa na madiwani wa kata ya Mlowa ,Itunundu, Mlenge na Ilolompya  pamoja na Mkurugenzi  wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa vijijini pamoja na mwenyekiti wa Halmashauri  ,mkuu  wa wilaya aliweza  kutoa maamuzi hayo kama njia ya  kuepusha mwanya wa ufisadi  kuendelea ndani ya Mbomipa. 



Hata  hivyo alipongeza hatua ya serikali ya wilaya ya Iringa chini ya mkuu wa wilaya  kwa kuivunja Halmashauri  hiyo na kuwa bila uamuzi  huo mradi  huo ungeweza  kufa

katika kikao cha kamati kuu ya Mbomipa na bodi ya wadhamini kilichofanyika juni 25 mwaka huu katika ukumbi wa Lutherani Centre pamoja na mambo mengine wajumbe walipokea taarifa kutoka kwa mwenyekiti juu ya wizara kumaliza mgogoro huo pamoja na kuwasilisha hati za maelewano kati ya bodi na kampuni ya Marera , mkataba wa uwekezaji kati ya kampuni ya Marera na Mbomipa mkakata ambao umeonekana kuwa ni feki baada ya uchunguzi .
Hata hivyo katika hati hizo mjadala mkali ulipata kuibuka baada ya wajumbe kukana kukaa na kampuni ya Marera Safari Lodge na kufikia makubaliano hayo kutokana na kutokuwepo kwa hati iliyosainiwa na bodi ya wadhamini walabodi haijawahi kumuagiza mtu yeyote aingie makubaliano ya aina hiyo kwa niaba na bodi .
Huku juu ya mkataba huo feki mkabata huo ni wa viongozi hao wawili makamu mwenyekiti na katibu wake wa Halmashauri ya Mbomipa na sio kwa ajili ya mradi huo wa Mbomipa ambao unataka bodi ya wadhamini kusaini mikataba kwa niaba ya Mradi huo wa Mbomipa na si vinginevyo. 
Hata hivyo alipongeza hatua ya serikali ya wilaya ya Iringa chini ya mkuu wa wilaya kwa kuivunja Halmashauri hiyo na kuwa bila uamuzi huo mradi huo ungeweza kufa.

Mwenyekiti  wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa Stevin Mhapa alisema kuwa hatua ya mkuu  wa wilaya  imelenga  kujenga mradi  huo na kuendelea  kunufaisha  wananchi kama ilivyokusudiwa na kuwa  kwa  sasa wanasubiri kuundwa kwa Halmashauri mpya itakayofanya kazi kwa misingi iliyowekwa.

No comments: