Friday, August 12, 2011

Benki ya jamii ya NMB yaipiga jeki WAMA



Mke wa Rais ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama Salma Kikwete akipokea mfano wa hundi ya shilingi milioni 10 kutoka kwa Mark Wiessing ambaye ni Afisa Mtendaji Mkuu wa benki ya NMB katika ofisi za WAMA Ikulu jijini Dar es Salaam leo. Fedha hizo zitatumia kwa ajili ya miradi ya uwezeshaji wa wanawake.
Mama Salma Kikwete (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mark Wiessing ambaye ni Afisa Mtendaji Mkuu wa benki ya NMB (kushoto) na ShyRose Banji ambaye ni Afisa Mahusiano (kulia) katika ofisi za WAMA Ikulu jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kukabidhiwa hundi ya shilingi milioni 10 na benki hiyo ya jamii.

No comments: