Tuesday, August 9, 2011

hivi hawa wamiliki wa vituo vya mafuta wanalindwa na nani?? Mbona wana kiburi kiasi hiki.!





Pichani ni Baadhi ya Wakazi wa jiji la Dar wakisaka mafuta mapema leo kwenye moja ya kituo kilichopo Sinza Mori.Hivi karibuni Serikali ilitoa tamka ya kwamba imemalizana na hawa wauza 'WESE' na kwamba wataanza kuuza mafuta hayo,atakae kaidi agizo la Serikali atachukuliwa hatua kali za kisheria,lakini la ajabu na kustaajabisha kabsaa hali imezidi kuwa tete kwa watumiaji wa mafuta hayo,na jamaa wameendela kuyabana mafuta yao,vituo vichache sana aghalabu vimeanza kuuza mafuta,Ninachojiuliza hivi hawa waliogoma kuuza hilo WESE kiburi chao wana kitoa Wapi??!Wanalindwa na nani??!
Kwa hisani ya Jiachie Blog

No comments: