Wananchi wa kijiji cha Ifunda kibaoni wilaya ya Iringa vijijini mkoani Iringa wamemwondoa madarakani mwenyekiti wao wa serikali ya kijiji kwa tiketi ya chama cha mapinduzi (CCM) Bw.Carius Kihwele(pichani) kwa tuhuma za ufisadi wa mali za kijiji hicho ikiwa ni pamoja na kugeuza mgodi ya chokaa wa kijiji kuwa mali yake.
Hatua ya wananchi hao kumtimua mwenyekiti huyo katika nafasi yake hiyo imekuja baada ya kuitishwa mkutano wa hadhara kwa ajili ya ufafanuzi wa tuhuma mbali mbali dhidi ya mwenyekiti huyo ambazo zilipata kuibuliwa na mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com na kupelekea mwenyekiti huyo kutoa vitisho kwa madai kuwa hakuna tuhuma kama hizo.
Hata hivyo mwenyekiti huyo katika hali ya kujiosha aliamua kuitisha mkutano ambao aliandaa baadhi ya wazee kwa lengo la kumlinda ila njama hizo ziligonga ukuta baada ya wananchi kumtaka kuachia ngazi katika nafasi hiyo kwa madai kuwa ameshindwa kuitumia vema.
KIhwele ambaye anatuhumiwa kwa matumizi mabaya ya nafasi yake ya uenyekiti wa serikali ya kijiji pia anadaiwa kutoa vitisho kwa wananchi wake kupitia vyombo vya habari kwa kuwaita wananchi wake kuwa ni wahuni na hawawezi kumfanya chochote .
Habari na Francis Godwin
No comments:
Post a Comment