Tuesday, August 23, 2011

Vodacom Miss Tanzania Walivyosherehekea Family Day Jana




Warembo wanaoshiriki katika shindano la Vodacom Miss Tanzania wakishuhudia Michael Jackson wa Bongo jinsi alivyokuwa akionyesha uwezo wa kuigiza kama Marehemu mwanamuziki wa Marekani Michael Jackson wakati wa sherehe yao ya Family Day Jana, ambapo warembo wanaoshiriki katika shindano la Vodacom Miss Tanzania walitembelewa na ndugu na jamaa zao kutoka sehemu mbalimbali, katika hoteli ya Girrafe iliyopo Mbezi pia walipata nafasi ya kucheza muziki na kundi la wanne star. 




Warembo wakicheza na Nyoka wa kundi la Wanne Star pamoja na wasanii wakundi hilo.


Msanii Wanne Star katikati akipiga picha na baadhi ya warembo wakati wa sherehe ya siku yao ya kukutana na wazazi, ndugu, jamaa na marafiki jana kwenye hoteli ya Girrafe Ocean View jijini Dar es salaam.



No comments: