Monday, August 1, 2011

Kamati Maalumu Ya Wanafunzi Wa Chuo Cha Ustawi Wa Jamii. Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari

Msemaji wa Kamati Maalumu ya Wanafunzi wa Chuo cha Ustawi wa Jamii, Boniface Benezeth, akisoma taarifa kwa waandishi wa habari (hawapo pichani), leo mchana jijini Dar es Salaam, kuhusu mgomo wa wanafunzi wa chuo hicho uliofanyika hivi karibuni.
KAMATI MAALUMU YA WANAFUNZI WA TAASISI YA USTAWI WA JAMII
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Ndugu Wanahabari,
JULAI 21, 2011, Taasisi ya Ustawi wa Jamii (ISW) ilisitisha masomo (kufunga chuo) kwa muda usiojulikana kutokana na kile kinachotajwa kuwa ni mgomo usio halali wa wahadhiri. Hali hii ya kufunga chuo (kusitisha masomo) imekuwa na madhara makubwa kwa wanafunzi (wanachuo) ikiwa ni pamoja na wengi kukosa malazi na hata wengine kushindwa kujikimu kimaisha huku wengine muda wao wa ruhusa kazini ukimalizika.
Kutokana na hali hiyo, baada ya tangazo la kusitisha masomo kutolewa na Kaimu Mkuu wa Taasisi, Mlwande Madihi mbele ya Mkutano Mkuu wa Wanafunzi ikiwa yapata saa 11:15 jioni, wanafunzi wote wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii katika Mkutano huo wakiongozwa na Rais wa Serikali ya Wanafunzi (ISWOSO) walikubaliana na kuunda Kamati Maalumu ya Dharura kwenda Dodoma kuwasilisha kilio cha wanafunzi kwa Serikali na hasa ikizingatiwa kuwa kutokana na vikao vya Bunge la 10 kuendelea, wakiamini kuwa viongozi hao wa Serikali (Mawaziri na Manaibu Waziri) watapatikana kirahisi hukohuko.
JULAI 24, 2011 (Jumapili), Kamati ilifika Dodoma na ikiongozwa na Kaimu Mwenyekiti Chrisant Mutatina; Makamu Mwenyekiti Mariam Saad na Katibu Kitamogwa Safari. Ikiwa Dodoma, ilikutana na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa na kisha ikakutana na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Lucy Nkya.
Siku iliyofuata Kamati hiyo ikiwa na wajumbe 10 ilikaribishwa katika Kikao cha Bunge na soma zaidi http://www.kwanzajamii.com

Picha na Victor Makinda

No comments: