Monday, August 1, 2011

TAIFA STARS KUPAMBANA NA CHAD KOMBE LA DUNIA 2014

Upangajimakundi ya mechi za mchujo kwa ajili ya fainali za Kombe la Dunia 2014nchini Brazil ulifanywa jana (Julai 30 mwaka huu) karibu na ufukwe waCopacabana jijini Rio de Janeiro nchini Brazil ukiongozwa na KatibuMkuu wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) Jerome Valcke.
Taarifailiyotolewa na msemaji wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF)Bw. Boniface Wambura imesema, Timu ya Tanzania (Taifa Stars) imepangwakundi C Kanda ya Afrika ambalo lina timu za Cote d’Ivoire, Morocco naGambia. Lakini kabla ya kuingia katika kundi hilo Stars italazimikakucheza raundi ya kwanza ya mchujo dhidi ya Chad.
Stars ikifanikiwa kuitoa Chad baada ya mechi mbili za nyumbani na ugenini zitakazochezwa kati ya Novemba 11-15 mwakahuu ndiyo itaingia katika kundi hilo la C. Pia mshindi wa kundi C ndiyeatakayeingia katika raundi inayofuata kabla ya kupata tiketi ya kwendaBrazil.
Starsni miongoni mwa timu 29 ambazo kwenye viwango vya ubora vya FIFA vyaJulai mwaka huu katika Afrika ziko chini ya timu 24 bora, hivyokulazimika kuanzia hatua hiyo ya kuchujana zenyewe kabla ya kuingiahatua ya makundi ambayo itachezwa kuanzia Juni 1, 2012 hadi Septemba10, 2013.
Kwamujibu wa viwango vya FIFA vya Julai mwaka huu, Tanzania iko katikanafasi ya 127 wakati Chad ni namba 158. Kwa upande wa Afrika, Tanzaniani namba 33 na Chad 43. Nchi 52 kati ya 53 za Afrika zimeingia katikamichuano hiyo ya Kombe la Dunia. Ni Mauritania pekee ambayohaikuthibitisha ushiriki wake.
Timu10 za juu kwa ubora barani Afrika ambazo zimeongoza makundi 10 yaAfrika katika upangaji ratiba ni Afrika Kusini, Tunisia, Cote d’Ivoire,Ghana, Burkina Faso, Nigeria, Misri, Algeria, Cameroon na Senegal.
Afrika ina nafasi tano kwenye fainali za Kombe la Dunia, huku Ulaya ikiongoza kwa kuwa nazo 13.
Habari Kwa Hisani Ya John Bukuku - Full Shangwe Blogu

No comments: