Saturday, August 13, 2011

kapumzike kwa amani mpiganaji mwenzetu Richard Masatu.



Marehemu akilazwa kwenye nyumba yake ya milele.
Mungu ailaze roho Merehemu mahali pema peponi-Amen
Mwakilishi wa ITV mkoani Mara George Marato akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa marehemu.
Mfanyabiashara maarufu jijini Mwanza Jack Masamaki akitoa heshima zake kwa mwili wa marehemu Richard Masatu.
==== ====== ========== ======== ======
Kwa niaba ya WAANDISHI WA HABARI wa Mwanza, nikiwa Mwenyekiti wao wa Kamati ya Maafa, napenda kuwashukuru sana wale wote ambao mmetupatia pole na kuonyeshwa kuguswa na Msiba huu. Asanteni.


Marehemu tumekamilisha safari yake ya mwisho kwa kumzika jana majira ya saa 11:26 jioni maeneo ya mitaa ya Barabara ya Majita Musoma, hapa ni nyumbani kwao kwa baba yake.
Pamoja na kumzika tumebaki na kitendawili kikubwa juu ya nini kimemkuta mwenzetu na kama kilikuwa kikihusiana na masuala yake ya kazi au laa! Tunaomba Mungu, atujalie uvumilivu ili tuliosalia tusikate tamaa ya kuendelea na kazi.


Binafsi ninaamini kile alichokuwa akikifuatilia tutafahamika kwani unapozuia watu kusema MAWE hupaza sauti juu. Wamemnyamazisha kusema kwa kumtoboa koromeo na ulimi ili asiseme, wamemvunja kifua chake ili kuharibu hifadhi ya siri alizokuwa nazo moyoni, wamemvunja mguu wa wake wa kushoto wakimzuia kuendelea kutembea kutafuta siri hizo. Zaidi ya hayo wamempasua Bandama na Pafu lake wakitaka asipumue. Haikuuwatosha pamoja na kumtoboa macho yake walimuwekea GUNDI (Super Glue) Machoni mwaka ili asione tena siri za uozo wao. Mungu atayafungua yote kwa vile ni Batili.


Aluta Continue.. Mapambano yataendelea na sasa ndiyo kwanza yameanza
Picha kwa hisani ya Gsengo,habari kwa hisani ya Frederick Katulanda.


No comments: