Sunday, August 14, 2011

KUTOKA BUNGENI DODOMA JANA NGELEJA AWASILISHA UPYA BAJETI YA WIZARA YAKE JANA


Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, akiingia kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma leo wakati akiingia bungeni kuwakilisha Makadirio na Mapato na matumizi ya wizara yake leo.
Mbunge wa Bumbuli, January Makamba, akichangia Makadirio ya Matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka wa Fedha 2011-2012, wakati wa kuwasilishwa kwa bajeti hiyo kwa mara ya pili Bungeni mjini Dodoma leo baada ya bajeti hiyo kukataliwa wakati ikiwasilishwa kwa mara ya kwanza bungeni hapo.
Mbunge wa Same mashariki Anne Kilango Malecela akichangia wakati wa kupitishwa kwa Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini Bungeni mjini Dodoma leo.
Msemaji wa kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe (kushoto) akijadiliana jambo na mbunge wa Ubungo (CHADEMA) John Mnyika, wakati wa majadiliano ya kupitisha hoja ya Makadirio na Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka wa fedha 2011-2012 Dododma leo.

Picha Zote na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO

No comments: