Friday, August 12, 2011

kutoka bungeni dodoma leo


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Uratibu na Bunge) William Lukuvi (aliesimama) akisoma muongozo leo Bungeni mjini Dodoma, ((kulia) ni Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja.
Mbunge wa viti maalumu (CCM), Zainab Vullu akichangia Hotuba ya Makadirio ya Matumizi ya Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo kwa mwaka wa Fedha 2011-2012 leo Bungeni mjini Dodoma.
Mbunge wa Jimbo la Ubungo (CHADEMA), John Mnyika akitaka ufafanuzi wa muongozo Bungeni Leo.
Mbungu wa Kawe (CHADEMA), Halima Mdee (kushoto) akinyoosha mkono ili aweze kupokelewa karatasi ya kuomba idhini ya Spika kuchangia hoja ya majadiliano ya Makadirio ya Matumizi ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa Mwaka wa Fedha 2011-2012 Bungeni mjini Dodoma leo.Kulia ni Mbunge Owenya (CHADEMA) .
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na wabunge wa Viti Maalum, Faida Bakari (kushoto) na Ritta Kabati kwenye viwanja vya Biunge Mjini Dodoma leo.
Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akifurahia jambo na Katibu wa Jukwaa la wahariri nchini,Neville Meena katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma leo.
Picha na Mwanakombo Jumaa - MAELEZO.

No comments: