Friday, August 12, 2011

Mgao wa Umeme Utakoma Disemba-TANESCOMeneja wa Mahusiano wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Badra Masood, akizungumza na waandishi wa habari leo mchana kwenye mitambo ya kufua umeme, Ubungo jijini Dar es Salaam. Badra alisema kuwa magao wa umeme utakoma kufikia mwezi Disemba mwaka huu. Akielezea mikakati mbali mbali ambayo TANESCO imefanya ni alisema kuwa ni pamoja na kukodisha mitambo yenye uwezo w kuzalisha Megawati 100, kutoka Kampuni ya Aggreco ya Mombasa, Kenya. Mitambo iliyowasili leo na kazi ya kuifunga itatarajiwa kuanza hivi hivi karibuni. Akielezea zaidi kuhusu ujio wa mitambo hiyo ya Aggreco, Badra alisema kuwa hii ilikuwa ahadi ya Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, alipokuwa akiwasilisha bajei ya wizara yake Bungeni hivi karibuni. Mipango mingine ya kumaliza mgao wa umeme ifikapo Disemba mwaka huu ni pamoja na kutumia mitambo ya Symbion yenye uwezo wa kuzalisha Megawati 112, na mitambo ya Jacobsen inayoendelea kufungwa hatua inayoipa Tanesco uhakika wa kumaliza kero ya mgao wa umeme mwezi Disemba mwaka huu.Moja ya kontena lenye mitambo ya Aggreco likiwasili leo mchana ubungo jijini Dar es Salaam.

Mitambo ya Aggreko ikishushwa, tayari kwa kufungwa.
 Picha zote na Victor MakindaNo comments: