MAJAMBAZI sita akiwemo mwanamke mmoja, ambao majina yao hayajajulikana, Wameuawa na Polisi jana majira ya saa usiku, katika tukio la kurushiana risasi baina ya majambazi hayo na Askari Polisi eneo la Mlima Sekenke Wilaya ya Iramba mkoa wa SIngida.
Majambazi hayo yamedaiwa yalikuwa yamejipanga kwa lengo la kuteka magari kwenye mlima huo wa Sekenke ili kupora mali za abiria na mizigo yao.
Mkuu wa upelelezi mkoa wa Singida, Ayubu Tenge, alisema kuwa majambazi hayo yamekamatwa yakiwa na bunduki aina ya SMG tatu na risasi 105 na mabomu ya kutupa kwa mkono saba na moja walilotumia kuwarushia polisi.
Alisema taarifa kamili itatolewa na kamanda wa polisi mkoa wa Singida leo mchana, juu ya tukio hilo.
Habari kwa hisani ya Sufiani Mafoto Blog
Habari kwa hisani ya Sufiani Mafoto Blog
No comments:
Post a Comment