Safu ya washambuliaji wa mbele ikiongozwa na kamanda Ras Makunja, akiwemo Diva Princess Bedi Beraca bella, ilikua na kazi ya moja tu...
...nayo kushambuliana jino kwa jino na washabiki, Washabiki nao walipopandisha mzuka wao wa mziki walirudisha mashambulizi ndani ya ulingo wa dansi!
Kiongozi wa bendi hiyo Kamanda Ras Makunja alikiongoza jukwaani kikosi chake ambacho mshambuliaji wa gitaa la solo Chris-B aka 'Mshenzi' wa gitaa,alikua akipereka makombora mazito ya milio ya nyuki katika gitaa.

Ilikua jumamosi ya asiye na mwana abebe jiwe ! katika tamasha la Afro-karibik, Robstock park, Frankfurt, Ujerumani.
Pata shika la nguo kuchaika kati ya ffu wa ngoma africa band na washabiki sugu mjini Frankfurt, katika onyesho ambalo washabiki walionyesha ubabe dhidi ya walinzi na kulikwea jukwaa baada ya kudatatishwa na mdundo wa Ngoma Africa band aka FFU

Wasikilize zaidi FFU at
www.ngoma-africa.com


No comments:
Post a Comment