Monday, August 15, 2011

MAKAMU WA RAIS MGENI RASMI KATIKA FAINALI ZA MASHINDANO YA QUR-AN JIJINI DAR


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa fainali za mashindano ya Qur-an kuhifadhi Juzuu 30, zilizofanyika jana kwenye Viwanja vya Shule ya Sekondari ya Al-Haramain jijini Dar es Salaam. Mshindi wa kwanza katika fainali hizo alikuwa ni Mariam Salum Mohamed, kutoka Tarbiyatul-Islamiyah Pemba.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi mshindi wa pili wa fainali za mashindano ya Qur-an, kuhifadhi Juzuu 30, Aisha Faki Khatib (18), kutoka, Istiqama Pemba, aliyeibuka na jumla ya Pointi 96 katika mashindano hayo yaliyofanyika jana katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Al-Haramain jijini Dar es Salaam. Kuliani ni Mufti Mkuu wa Tanzania, Ally Mkoyo Gole.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi mshindi wa kwanza wa fainali za mashindano ya Qur-an, kuhifadhi Juzuu 30, Mariam Salum Mohamed (15) kutoka Tarbiyatul-Islamiyah Pemba, aliyeibuka na jumla ya Pointi 97 katika mashindano hayo yaliyofanyika jana katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Al-Haramain jijini Dar es Salaam. Kuliani ni Mufti Mkuu wa Tanzania, Ally Mkoyo Gole.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi mshindi wa kwanza wa fainali za mashindano ya Qur-an, kuhifadhi Juzuu 10 (Tahqeeq), Mohamed Salum (12) kutoka, Darul , aliyeibuka na jumla ya Pointi 98 katika mashindano hayo yaliyofanyika jana katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Al-Haramain jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mufti Mkuu wa Tanzania, Ally Mkoyo Gole.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi mshindi wa tatu wa fainali za mashindano ya Qur-an, kuhifadhi Juzuu 30, Shaame Said Shaame(18) kutoka, Ibun Jazary Vikindu, aliyeibuka na jumla ya Pointi 93 katika mashindano hayo yaliyofanyika jana katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Al-Haramain jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mufti Mkuu wa Tanzania, Ally Mkoyo Gole.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi kutoka kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake, Baraza Kuu la Kiislam (BAKWATA), Shamim Khan, wakati alipokuwa mgeni rasmi katika mashindano hayo yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Shule ya Sekondari Al-Haramain jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Mufti Mkuu wa Tanzania, Ally Mkoyo Gole. Picha na Muhidin Sufiani-OMR.

No comments: