Tuesday, August 23, 2011

Mbunge wa baraza la wawakilishi Mussa Khamis silima afariki dunia




Hayati Mussa Khamis Silima

Mbunge Mussa Khamis Silima wa Baraza la Wawakilishi, Zanzibar, amefariki dunia.
Akitoa taarifa hiyo Mh. makinda amesema , asubuhi amesema kuwa alitoa taarifa kuhusu ajali ya Mbunge mwenzetu eneo la Nzuguni na kwamba mke wake alifariki papo hapo,
“Na nilisema kwamba dereva wake na Silima walipata majeraha makubwa na wamepelekwa Muhimbili kwa matibabu zaidi.
“Nimepokea taarifa kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kuwa Mheshimiwa Mussa Khamis Silima amefariki dunia muda mfupi uliopita/

"Kwa mujibu wa kanuni ya 149 ya Bunge toleo la 2007, naahirisha shughuli za Bunge mpaka kesho saa tatu asubuhi,” alisema na kuomba kukutana na Kamati ya Bunge ya Uongozi kuzungumzia na
kupanga kuhusu msiba huo.



Habari zinasema hayati Silima alipotaarifiwa kuhusu kifo cha mkewe leo baada ya kufichwa toka jana, hali yake ilibadilika ghafla na muda mfupi baadae alifariki dunia.


Hayati Silima akiwa na mkewe Mwanaheri dereva, walipata ajali mbaya katika eneo la Nzuguni, Dodoma juzi usiku wakitokea Dar es Salaam baada ya kuhudhuria mazishi ya shemeji yake na kusababisha kifo cha mkewe. Yeye na dereva walijeruhiwa vibaya na kuhamishiwa Muhimbili kitengo cha Mifupa MOI kwa matibabu zaidi.
Habari na Issa Michuzi Blog


No comments: