Tuesday, August 2, 2011

MBUNGE WA CCM MBEYA AZOMEWA NA WAPIGA KURA WAKE


MKUTANO wa hadhara ulioitishwa na mbunge wa Mbozi Mashariki,Godfrey Zambi (pichani)(CCM),mwishoni mwa wiki kwa lengo la kuwashukuru wananchi wa hilo kwa kumchagua,uligeuka shubiri baada ya wananchi kuanza kuzomea na wengine wakimtamkia hadharani kuwa anatakiwa kujiuzuru kutokana na kutuhumiwa za kuomba rushwa na yeye kuka kimya.


Tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Stendi Kuu ya zamani mjini Vwawa, baada ya wananchi hao kukerwa na kitendo cha kufika hapo na kuanza kuhutubia bila kufafanua tuhuma zilizotolewa dhidi yake kuwa aliomba rushwa.
Pia wananchi hao wamemtaka Mwenyekiti wa kamati ya maadili ya Bunge,ambaye ndiye Spika bunge, Anne Makinda,kuharakisha kutoa taarifa ya tume iliyoundwa kuchunguza tuhuma hizo ili waweze kuchukua maamuzi dhidi ya mbunge wao huyo ambaye ni miongoni mwa wabunge wa CCM wanaotuhumiwa kuomba rushwa wakiwa wanatekeleza majukumu ya kamatii ya bunge ya hesabu ya serikali za mitaa.
“Hivi juzi tulisikia bungeni kuwa wewe na wenzako watatu mnatuhumiwa kuomba rushwa katika moja ya halmashauri nchini hivyo tulitarajia ulivyofika hapa ungeanza kutuomba radhi kwa jambo hilo,lakini umeanza kujieleza kwa mambo mengine,je unaweza kutuambia kuwa sasa unaweza kuachia ngazi (kujiuzuru) kama mwenzio …akimaanisha mbunge wa Igunga Rostam Azizi ”. alihoji mmoja wa wananchi hao Lameck Mwaipaja.
Hata hivyo wakati Mwaipaja akiendelea kuuliza swali hilo pamoja na mengine wananchi wenzake walilipuka kwa kelele wakimshangilia kuonyesha kumuunga mkono kwa hoja hiyo ya kutaka mbunge wao ajiuzuru.
Aidha, mwananchi mwingine alijitaja kwa jina la Abraham Msyete,alimbana mbunge huyo na kutaka kujua ni sababu gain ambazo zimesababisha kuonyesha machachari ya kuibana serikali juu ya bei ya mafuta ya taa badala yake wamekaa kimya na kuacha wananchi wakiumia.
Akijibu tuhuma hizo, mbunge Zambi alisema kuwa yeye hawezi kujiuzuru kwa kuwa tuhuma hizo zilizoytolewa na Kafulila zilikuwa ni hisia na kwamba Kafulila alifanya hivyo kwa lengo la kutafuta umaarufu wa kisiasa kwa kuwa tuhuma zote zilikuwa katika mfumo wa hisia tu.
“Ngoja niwaambie ukweli,mimi na wenzangu wa CCM ,Muhita (Kondoa) na Baduwel (Bahi) TULIPOFIKA Korogwe wenzetu hao wanaotoka upinzani akiwemo Kafulila walikataa kufikia kwenye Hoteli tulizolipiwa eti kwa madai ni rushwa,na siku ya pili walipotuona sisi tukiwa tumesimama na Mkurugenzi na mweka hazina wakadai eti tulikuwa tunaomba rushwa”.
Majibu hayo ya Zambi yaliamsha hisia kali ambapo wananchi walipiga kelele za kuzomea hali iliyomlazimu mbunge huyo kutoa maneno makali “ Jamani kama mtu hakuta kuja kunisikiliza ni bora aondoke maana huu ni mkutano wangu na mimi ndio mbunge wa Mbozi kama kuna watu wanafikiri vingine wasubiri 2015”alisema Zambi.
Awali kabla ya mkutano huo ulioitishwa na mbunge huyo kwa lengo la kuwashukuru wananchi na kufanyika katika viwanja vya Stendi Kuu ya zamani,ulitawaliewa na rabsha za hapa na pale ambapo baadhi ya wananchi walikuwa na bango yaliyomtaka mbunge huyo kujiuzuru hali iliyo lilazimu jeshi la polisi kuongeza nguvu katika mkutano huo.
Hivi karibuni akiwa kwenye vikao vya bunge la bajeti linaloendelea mjini Dodoma,mbunge wa kasulu David Kafulila aliwatuhumu wabunge watatu wa CCM , Omar Baduwel,Zubein Muhita,pamoja na Zambi kuwa wakiwa katika moja ya halmashauri wabunge hao waliomba rushwa.

No comments: