Monday, August 1, 2011

Mgao Wa Umeme, Wataalamu Wasikilizwe; Asema Mbatia

Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia, akizungumza na makada wa chama hicho wa mkoa wa Dar es Salaam mapema mchana wa leo katika ukumbi wa TRIZ Motel,Mbezi, jijini Dar es Salaam, kuhusu hali ya kisiasa nchini na changamoto za kiuchumi.Mbatia alisema kuwa suala la umeme linachukuliwa kisiasa na wataalamu hawapewi nafasi ya kupanga na kuamua nini kifanyike kumaliza mgao wa umeme.Akizungumzia juu ya kiti cha Spika na 'kashikashi' zinazotokea bungeni, Mbatia aliseama kuwa Spika Makinda anayumbishwa na Chama chake cha CCM, Kwani yeye binafsi haoneshi kuwa ana maamuzi na kubaki kusikiliza maelekezo kutoka kwa vigogo wa CCM.
Makada wa chama waliohudhuria mkutano huo.
Picha zote na Victor Makinda

No comments: