Thursday, August 18, 2011

MIGAMBO WAKAMATWA WAKIPOKEA MLUNGULA KATIKA STENDI YA UBUNGO







Afisa wa Takukuru akijaribu kuwatuliza wananchi ili wasifanye fujo baada ya kuwakamata wadada hao.






Kuna wanamwake wawili jana mchana wamekamatwa kwa kosa la kupokea Rushwa kwa moja kati ya wafanyabiashara maeneo ya stendi ya Ubungo ndani. Kwa kawaida wadada hao ambao nilifanikiwa kujua kwa majina yao ya Anna n Asia walikamatwa kwa kosa lakupokea Rushwa na kusemekeana kuwa ni kawaida ya wadada hao kupokea Rushwa maeneo hayo kwa kutumia uongozi walionao wa askari Jiji.






Watuhumiwa wa kupokea rushwa, wadada hao Asia na Anna wakiwa chini ya ulinzi baada ya kukamatwa wakipokea mshiko katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani cha Ubungo.






Ni sehemu ya watu wakiandamani kuwasindikiza watuhumiwa na wengine ni wasafiri wa mikoani wakiwa wamekatisha shughuli zao hili kushuhudia tulio hilo.






Msafala uliishia hapo jamani.

---
Katika tukio la kushangaza lililotokea jana katika Stendi ya mabasi yaendayo mikoani ya Ubungo, migambo wawili kama unavyowaona hapo pichani, walijikuta wakiwa hatiani baada ya kuomba kiasi cha Sh.20,000 kutoka kwa wapigadebe ili wasiwakamate.

Tukio hilo lililovuta hisia za watu wengi na zaidi wapigadebe hao ambao kila kukicha hawaishi kumwaga machozi ya kukamatwa na migambo hao, lilipelekea migambo hao kutimiza arobaini zao.

Mtego huo uliokuwa umewekwa na baadhi ya wapigadebe hao, na kufanikisha azma yao hiyo, uliwafanya migambo hao wajione wadogo kama kidonge cha Piliton na zaidi pale walipokuwa wakizomewa na wapigadebe zaidi ya mia mbili waliwazunguka.

Inasemekena kutokana na tabia yao ya kuomba mlungula huo kila kukicha, tayari baadhi yao wamefungua Baa ndani ya Stendi hiyo na hivyo kula maisha kiulaini kupitia jasho la vijana hao ambao kila kukicha hawaishi kukumbana na misukosuko.

Hii itakuwa fundisho kwa migambo hayo na wenzao wanapita mitaani kila siku na kuwapokonya wamachinga vitu vyao kwa madai ya kukiuka taratibu za Jiji hili, hususani maeneo ya Kariakoo na Posta.

Habari kwa Hisani ya Habari na Matukio Blog

No comments: