Tuesday, August 16, 2011

Simba Cement Yadhamini Kambi Ya Tennis


Meneja Uendeshaji wa kampuni ya Tanga Cementi,Erick Westerberg,akielezea kwa waandishi wa habari leo mchana katika viwanja vya Gymkhana, namna kampuni hiyo ilijidhatiti kudhamini kambi ya watoto wadogo wachezaji wa mpira waTennis. Westerberg alisema kuwa Simba Cement, imeamua kudhamini ´kambi ya mchezo huo kwa lengo la kukuza vipaji vya watoto na kwa kuthamini umuhimu wa michezo nchini hususani kwa rika la vijana na watoto.
Kocha wa kimataifa waTennis,Fabrizio Coldarone, akizungumza´na waandishi wa habari leo kuhusu ujio wake na nini Watanzania watarajie kutoka kwake.Alisema kuwa atajitahidi kuwafundisha wachezaji hao chipukizi jinsi ya kucheza mchezo huo kwa kiwango cha Kimataifa.

Mwenyekiti wa Baraza la Michezi la Taifa (BMT), akizungumza leo mchana katika ufunguzi rasmi wa kambi ya mchezo wa Tennis, katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam. Kanali kipingu alisema kuwa hakuna namna nyingine ya kupata wachezaji bora na timu bora zidi ya kuwekeza michezo kwa watoto. Hivyo alitoa ushauri kwa Serikali na wadau wapenda michezo kuelekeza nguvu zao katika kuibua na kukuza vipaji vya michezo vya watoto.

Baadhi ya wachezaji chipukizi wa Tennis, wakiwa katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam leo mchana. 
Picha na zote na Victor Makinda







No comments: