Tuesday, August 16, 2011

ZANTEL YAKABIDHI ZAWADI KWA WASHINDI WA PROMOSHENI YA ZARI SMS MKOANI MBEYA


Kushoto ni Meneja wa mauzo Kanda ya Nyanda za juu Kusini kupitia kampuni hiyo ya Zantel Bwana Killian Nango akimkabidhi fedha Bwana Titto Waya ambaye ni mshindi wa Shilingi Milioni moja alizopata kutokana na bahati nasibu ya Zari SMS.

Kampuni ya Simu ya mkononi ya Zantel 'Ongea zaidi' nchini Kanda ya Nyanda za juu Kusini, imemkabidhi shilingi Milioni moja tasilimu mshindi wa bahati nasibu ya Zari Sms inayoendeshwa na kampuni hiyo.

Fedha hizo zimekabidhiwa leo katika ofisi ya kanda ya kampuni hiyo ya Zantel iliyopo mkoani Mbeya.

Akikabidhi fedha hizo kwa mshindi huyo, Meneja Mauzo kanda ya nyanda za juu kusini Killian Nango, alisema kuwa mshindi huyo amebahatika kupata kiasi hicho cha fedha baada ya kutuma meseji nyingi katika bahati nasibu hiyo.

''Kampuni yetu licha ya kuwa na gharama ndogo za huduma ya kupiga simu katika mitandao yote hapa nchini, pia ni kampuni yenye uhakika wa kutoa zawadi kwa wateja wetu pindi inapotokea promosheni yeyote hakika hatuna ubabaishaji wala usumbufu kwa wateja wanaobahatika akiwemo huyu wa leo na mwingine pia amebahatika kupata kompyuta ya kiganjani(Laptop)''amesema Meneja huyo.

Kwa upande wake mshindi wa shindano hilo Titto Waya(33) amesema kuwa amejisikia furaha kupatiwa kiasi hicho cha fedha kutoka kampuni hiyo na kwamba hata ndugu na jamaa zake wamehamasika kutumia mtandao huo wa simu baada ya kupata taarifa ya kushinda kwake.

''Najisikia furaha sana kushinda hii Milioni moja na hii ni mara yangu ya kwanza kupata zawadi kama hii ya promosheni ingawa nimewahi kucheza bahati nasibu nyingi katika makampuni mengine ya simu'' alisema kwa furaha mteja huyo wa Zantel.

No comments: