Tuesday, August 16, 2011

SWEDEN YATOA MSAADA WA MIL 120 KWA MAKUMBUSHO NA NYUMBA YA UTAMADUNI

Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dkt Paulo Mswemwa akipewa pongezi na Balozi wa SPIDER nchini baada ya kupokea msaada toka SPIDER.
Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dkt Paul Msemwa akimshukuru Mkurugenzi wa SPIDER Dkt Paula Uimonen kwa kuipatia msaada Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni – Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dkt Paul Mswemwa, Mkurugenzi wa SPIDER Dkt Paula Uimonen baadhi ya viongozo wa Taasisi zilizo saidiwa na zitakazo saidiwa na SPIDER.
viongozi wa Taasisi zilizo patiwa Misaada na zinazo tarajiwa Kusaidiwa na SPIDER kutoka kulia ni Balozi wa SPIDER - Tanzania Theophilus Mlaki, Mkurugenzi mtendaji wa ITIDO Jacob Mtalitinya, Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dkt Paul Mswemwa, Mkurugenzi wa SPIDER Dkt Paula Uimonen, Mkuu wa kitengo cha Kompyuta cha Tume ya kaki za binadamu na Utawala Bora Wilfred Wrioba na Mwanamuziki Vitali Maembe.Picha zote na Sixmund J.Begashe wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni.

Progaram ya ICT katika nchi zinazo endelea inayo ratibiwa na Idara ya Kompyuta ya Chuo Kikuu cha Stockholm Sweden (SPIDER) imetoa msaada kwa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni ya Dar Es Salaam wa shilingi Milioni 120 (SEK 500,000) kwa ajili ya kutumia Teknohama (ICT) katika kukusanya, kutunza na kutumia Urithi wa Utamaduni wa Mtanzania.

Makubaliano hayo yametiwa saini kati ya Uongozi wa SPIDER na Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni, ambapo Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni itatumia msaada huo kununulia vifaa vya Studio ya Kurekodi na kuzalisha Video, Muziki na Sauti. Aidha, msaada huo utatumika pia kununulia Kompyuta na kamera ambazo zitatumika na wadau kuiwekea kumbukumbu ya matukiombalimbali na kupata taarifa za kuhusu urithi wa Tanzania unaohifadhiwa na Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni.

Mkurugenzi wa SPIDER Dr Paula Uimonen alifurahishwa na jitihada za uongozi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni chini ya Uongozi kwa kusimamia vyema mradi mkubwa wa shirika hilo na ni imani yake kuwa ushirikiano huu utawanufaisha wananchi wa nchi hizi mbili na hasa vijana.

Dr Uimonen alizitaka Taasisi nyingine za kiserikali na zile sisizo za kiserikali ambazo zimepatiwa Msaada na SPIDER, kuiga mfano wa Uongozi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni wa matumizi mazuri ya fedha za miradi zinazo tolewa na wahisani kwa ajili ya maendeleo ya Taifa hili na si kujinufaisha wenyewe, ameahidi kuwa ofisi yake itakuwa karibu sana na Taasisi zote zilizo pewa fedha na SPIDER ili kuwahikisha zinatumika kwa malengo yaliyo kusudiwa.

Ujenzi wa mradi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni ambao umefadhiliwa na Selikali ya Sweden na Tanzania unatarajiwa kumalizika Mwishoni mwa mwezi huu na kuzinduliwa Rasmi Desemba, 2011 sambamba na maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Jamuhuri ya Tanzania.

Kutokana na Mradi tayari kuna ukumbi wa Maonyesho kwa watazamaji zaidi ya 500, Studio ya kurekodi Muziki na Sauti, Maktaba ya Kisasa, sehemu kwa ajili ya watoto kujifunzia kazi mbali mbali za mikono, chumba maalum cha Masimulizi ya hadithi kwa watoto, kumbi kwa ajili ya maonesho ya mikusanyo ya Kibaiolojia, Mila na Desturi, Historia, Chimbuko la Mwanadamu, Chumba maalum cha kuhifadhia Mikusanyo, Vyumba vya Utafiti, Ofisi, Duka la Zawadi na Kantini kwa ajili ya vyakula na vinywaji.

Mkurugeni wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dr Paul Msemwa aliushukuru Uongozi wa Spider na kusema msaada huu umekuja wakati muafaka ambapo shirika limejipanga kutoa elimu kwa jamii kuhusu Utamaduni na Sayansi.

No comments: