Mafundi wakisambaza nyaya za mkongo wa Taifa ambao kwa sasa unasambaa kila mahali nchini na kuisogeza Tanzania karibu kabisa na njia kuu ya mawasiliano ya kasi duniani. Mpango mkubwa wa awali wa mkongo huo ulikuwa ni kusogezwa hadi mipakani ili nchi jirani ziweze kununua huduma hii kutoka kwetu, jambo ambalo limefanikiwa kwa kiwango kikubwa kwani juzi tu tayari Rwanda wameweka nia ya kuunganishwsa haraka iwezekanavyo. Nchi zingine zinazotegemewa kujiunga na mkongo wetu ni pamoja na Malawi, Zambia, Congo na Burundi. Hivi tunavyoongea wilaya takriban 17 nchini zimeshaunganishwa na mkongo wa Taifa na kazi inaendelea kwa kasi ili ufike katika kila wilaya ifikapo mwishoni mwa 2012.
Picha kwa hisani ya Michuzi Blog
Picha kwa hisani ya Michuzi Blog

No comments:
Post a Comment