Thursday, August 4, 2011

YALIYOTOKEA KATIKA BENKI YA CRDB TAWI LA AZIKIWE POSTA MPYA JANA

Askari Polisi wakimdhibiti kijana ambaye alifanya fujo kwakupiga mawe vioo vya benki ya CRDB tawi la Azikiwe, Posta Mpya, Dar esSalaam jana na kusababisha wateja na wananchi kukimbia ovyo. (PICHAZOTE NA KASSIM MBAROUK)
wewe unajifanya fara sio, basi mimi ni fara zaidi...
Kaa chini...arrraaaaah!
Na Kamanda Mwaikenda

TAFRANI kubwa ilitokea jana katika Benki ya CRDB, tawi laAzikiwe, baada ya kijana mmoja aliyehisiwa kuwa jambazi kurusha mawekwenye vioo vya benki hiyo na kusababisha wateja kukimbia ovyowakidhani wamevamiwa.
Tukiohilo lilitokea jana mchana, ambapo kijana huyo anayedhaniwa kuwa akiliyake imeathirika kwa kubuia dawa la kulevya 'Teja' kurusha mawekuelekeza kwenye jengo hilo na kuvunja vioo.

Baadhiya wateja walianza kutimua mbio kutoka nje huku wengine wakilala chinikuhofia maisha yao.Baada ya kuona hivyo, Polisi waliokuwa kwenye lindola benki hiyo, walifyatua risasi juu wakidhani majambazi wamevamiabenki hiyo. Lakini baada ya muda walimuona kijana huyo aliyekuwakatikati a Barabara ya Azikiwe karibu na kituo cha Daladala cha PostaMpya, akiendelea kurusha mawe.

Polisi walimuendeana kufanikiwa kumdhibiti na kuanza kumpatia mkong'oto wa nguvu, hukuwanachi wenye hasira wakitaka nao waruhusiwe kumwadhibu.
Ndaniya benki hiyo hali ilikuwa shaghalabaghala, kwani mitungi ya maua nabaadhi ya nyaraka zilitawanyika ovyo, huku wakioneakana baadhi yawateja wakiwa wamezirai na wengine wakilia baada ya kupotelewa nanyaraka muhimu za benki vikiwemo kadi na fedha taslimu.
Wakatitukio hilo ilitokea, pia hali haikuwa nzuri kwa wafanyakazi wa benkihiyo, kwani baadhi walisikika kuwa walipatwa na hofu kubwa kiasi chabaadhi yao kukimbilia kujificha vyooni na kuacha kaunta zao.
Habari Kwa Hisani Ya Issa Michuzi - Michuzi Blogu

No comments: