Friday, August 19, 2011

WAHADHIRI 21 USTAWI WA JAMII WAACHISHWA KAZI




Profesa Msambichaka

Na Lukwangule

Bodi ya Magavana ya Taasisi ya Ustawi wa Jamii imewafukuza wahadhiri 21 wa chuo hicho kutokana na kuendesha mgomo unadaiwa sio halali.

Mwenyekiti wa Bodi ya Magavana Profesa Lucian Msambichaka, amesema uamuzi huo ulifikiwa Agosti 17, mwaka huu baada ya kufanyika kwa kikao cha Bodi.

Kwa mujibu wa taarifa wahadhiri hao wamefukuzwa kwa kukaidi maagizo ya mamlaka za juu.

Agizo la kutaka Taasisi hiyo ifunguliwe mara moja lilitolewa hivi karibuni na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ambaye aliigiza Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inayoisimamia Taasisi hiyo kushughulikia suala hilo mapema iwezekavyo.

Wahadhiri waliofukuzwa kazi ni Faustine Nzigu, Rindstone Ezekiel, Mariana Makuu, Aziel Elinipenda, Deodatus Mkumbe, Daud Chanila, Viscal Kihongo, Elizabeth Bitegela, Joseph Sunguya, na Constantine Njalambaya.

Wengine ni Mwajuma Hussein, Rita Minga, Caroline Mutagwaba, Elia Kasalile, Marwa Phanuel, Adrophina Salvatory, Kinswemi Malingo, Suzana Nyanda, Machumbana Michereli, Warioba Nyamoni na Yassin Mwita.
Habari kwa Hisani ya Michuzi Blog



No comments: